Burudani

Vanessa Mdee alilipwa kuonekana kwenye video ya Jux, ajibu tena swali la kama ni kweli ni wapenzi (Exclusive Audio)

Vanessa Mdee hakutokea kwenye video ya ‘Sisikii’ ya Jux bure.

10895144_1539207049668717_2055576873_n

Jux alilazimika kumlipa Vee Money gharama za hitmaker huyo wa ‘Hawajui’ kuonekana kwenye video hiyo iliyofanyika nchini China.

“Ni kweli alinilipa,” Vanessa ameiambia Bongo5.

“I don’t like to do videos, sio kitu ambacho nafanya and hiyo ilikuwa challenge kwangu. Alinipa hela ambayo ingeweza kunisaidia kuwezesha hiyo role ya lead actress kwenye video,” ameongeza Vee.

Vanessa ameongeza kuwa ilikuwa ni kitu alichokifurahia kufanya video hiyo kwakuwa siku zote hupenda kufanya kazi na waongozaji wapya na kwamba hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kufika China.

https://www.youtube.com/watch?v=0IYsRm84KZU

“It was nice kufanya kazi na Zed Benson. Ni kijana ambaye yuko very alert na ana ideas nyingi sana na kazi yako kama unavyoiona, ni kazi nzuri anafanya. Pamoja na hayo it was my first time in China so nimepata experience ya kuona culture tofauti. Wako very professional na ni nchi ambayo imeendelea vizuri.”

Katika hatua nyingine, akijibu tena swali la kama ni kweli yeye na Jux ni wapenzi, Vanessa amesema anapendelea kutoweka wazi mambo yake binafsi.

“I actually I like to keep my private life private,” amesisitiza.

“Nadhani kuna baadhi ya mambo ambayo hayahitaji majibu.”

Msikilize zaidi hapo chini.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents