Uncategorized

Vanessa Mdee alikuwa wapi muda wote huu bila kuimba? Wow! She has the most beautiful voice (Me and You)

Ni ngumu kuelewa kipaji cha Vanessa Mdee kinaishia wapi. Kila kukicha mtangazaji huyu wa kimataifa ambaye anaiwakilisha Tanzania katika mtandao mkubwa wa TV duniani, MTV Networks akiwa ni VJ wa MTV Base, amekuwa akivumbua kipaji kimoja baada ya kingine. Ni mtangazaji mzuri wa lugha zote. Wapo watangazaji wachache wenye uwezo wa kuswitch lugha na kutangaza vizuri bila kuathiri lugha nyingine.

Akitangaza Kiingereza, lugha ambayo huitumia zaidi utampenda Vanessa. Ni kama alizaliwa huko huko kwa wenye lugha yao. Akitangaza Kiswahili napo huwezi kusikia kuathiriwa kokote kwa Kiingereza anachokitumia kila siku, mswahili haswaa! Then hivi majuzi watu wengi wamekuja kugundua kuwa kumbe Vanessa Mdee ni mwanamuziki pia.

Well, tunafahamu watangazaji wengi muziki upo kwenye damu yao kwakuwa hata Ray C na Lady Jaydee walianzia huko. Kushirikiswa kwake kwenye ngoma ya AY, Money iliyotoka wiki mbili zilizopita kuliwaamsha wengi. Japokuwa alisikika sehemu chache tu, wajuzi wa muziki waligundua kuwa ndani ya Vanessa kuna msanii.

Pengine ndio maana Ommy Dimpoz kwa kujiamini ameamua kumshirikisha Vee kwenye ngoma yake iliyotoka jana (November 15) iitwayo Me and You!! Hapo sasa ndipo kila mmoja amebaki mdomo wazi kwamba kumbe this beautiful girl can sing ahhhh!

Vanessa killed this track! Ana sauti tamu mtoto huyu. Ukiwa umelala na ukashtukizwa tu useme ni msichana gani anayesikika kwenye ngoma hii mpya ya Ommy, itakuchukua muda kumtaja zaidi ya kusema huenda Ommy kamshirikisha msanii mkubwa wa Nigeria. Level kama za Waje aliyeimba ‘Do me’ ya P-Square.

Yaani kwa maana nyingine ni kuwa Vanessa Mdee si mwanamuziki anayependa tu kuimba bali muziki unataka uimbe, anaweza. Ni rahisi sana kwa Vanessa sasa kubadilika kutoka kuwa mtangazaji mashuhuri na kuwa mwanamuziki wa kimataifa anayetafutwa kwa udi na uvumba.

Hatuwezi kuacha kumpa haki yake Ommy Dimpoz kwa kazi hii nzuri. Labda tukukumbushe tu kuwa katika muziki ni ngumu sana msanii kutoa nyimbo tatu zinazofuatana na kila mpya iiizidi ya zamani. Ommy ameweza hilo. Unakumbuka Nai Nai ilivyohit?

Wale ambao walimfahamu Ommy kwa mara ya kwanza kupitia ngoma hiyo walijikuta wakisema kuwa ngoma hiyo imehit sababu amemshirikisha Ali Kiba. Alipotoa Baadaye, waliokuwa na wasiwasi na uwezo wake wakampa salute kuwa kijana habahatishi.

Kisha sasa Ommy ambaye jina lake halisi ni Omary Faraji Nyembo amekuja na monster hit hii, Me & You ambayo tunaongea kwa kujiamini kuwa tafika mbali sana. Kikubwa tu Ommy asifanye kosa la video (video ya kawaida sana kama si mbaya) kama alilolifanya kwenye Baadaye. Me & You inahitaji kioo kikali haswaa. Ngoma kama hii ikipata video kama anazofanya Clarence Peters wa Nigeria, itafika mbali kuliko anavyoweza kudhani. Me and You ni hit.It’s a club banger, ikichezwa lazima utikise kichwa kama utaona uvivu kuinuka na kwenda kwenye stage!

Pongezi zingine ziende kwa mpishi wa kibao hiki aitwaye Imma the Boy wa studio za THT. Kazi nzuri.

Na si peke yetu tulioshangazwa na uwezo huu wa Vanessa na uzuri wa wimbo huu pia:

Deo Hugo: Bonge la song, @VanessaMdee sauti yako dah

Lusajo LM; Been listening to @ommydimpoz featuring @VanessaMdee Me n U and I must admit it is a catchy tune. Good one

Teddy Kalonga Haight: Wow!! Nice track

EmmyRemman: Me & You @VanessaMdee and Ommy Dimpoz wow! cant stop listening to tha song! Love it

Ncha Kalih: Hii ngoma ni kali sanaaa… @VANESSAMDEE i told you you can do it

Ben Pol: Anko chulu chulu chululeee nyimbo mpya kalii sanaaa yani international standards keep it up

Usikilize hapa:

Download Here

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents