Bongo Movie

Uwoya: Range Rover nimeipata kwa njia nyingine sio sanaa, akiri ‘maisha ya Instagram’ kwa waigizaji hayatokani na sanaa

Baadhi ya wasanii wa kike wa Bongo movie wamekiri kuwa maisha mazuri na ya kifahari ambayo huwa wanatuonesha kwenye Instagram, hayatokani na kipato wanachokipata kupitia sanaa ya uigizaji kwasababu ni kidogo kulinganisha na maisha hayo.

Irene-range2

Irene Uwoya ni miongoni mwa waigizaji waliokiri hilo kupitia kipindi cha ‘Take One’ cha Clouds Tv, na kuongeza kuwa majina wanayoyajenga kupitia sanaa ndio yanayowawezesha kupata fursa zinazowasaidia kuwa na maisha mazuri na sio kipato cha kuigiza.

Irene-range1

Mwaka jana Uwoya aliwahi kushare picha za gari lake alilokuwa amenunua aina ya Range Rover- evoque nyeusi, lakini amekiri kuwa gari hilo hakulipata kwa pesa ya movie.

“Sipendi kuwa muongo napenda kuwa mkweli, kweli nafanya sanaa inaniingizia hela, lakini mambo ya evoque nimeyapata kupitia njia nyingine,”alisema Uwoya. “ambayo pia sanaa ilinisaidia nikaipitia hiyo njia…boss wangu Ruge alisema fursa, unaitumia fursa, kwahiyo nilipata fursa ya kuingia kwenye sanaa na mimi nikaitumia hiyo fursa kupata vyanzo vingine vya hela nikainunua ile gari”.

Kama hiyo haitoshi Uwoya ameongeza kuwa sio Range Rover pake yake ambayo iko chini ya himaya yake, “sio moja Zamaradi yako mengi mengi mno, kwahiyo unatumia fursa”. Upo?

Hata hivyo pamoja na Zamaradi kumbana mrembo huyo ataje hiyo ‘njia nyingine’ jibu lilikuwa hili: “Zamaradi hiyo ni siri yangu nikianza kukwambia si wataniiga, haiwezekani siwezi kukwambia”.

Haya kazi kwenu wasanii wa muziki kutumia fursa kupitia majina yenu kupata ‘njia nyingine’ ya kupata maisha mazuri, ila hakikisha iwe ni njia safi na halali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents