Burudani

Utashangaa jinsi remix ya Zigo ilivyorekodiwa Afrika Kusini

AY na Diamond wanasherehekea mafanikio yaliyokuja ndani ya muda mfupi ya remix ya Zigo, lakini haikuwa rahisi kuingia studio na kuirekodi.

Cha kufurahisha ni kuwa AY na Diamond walipanda ndege kwenda Afrika Kusini kushoot video ya wimbo huo wakati hata remix haijafanyika bado.

Sababu kubwa ni kuwa walipofika Afrika Kusini wote walijikuta wakiwa busy na mambo yao mengi na hivyo ratiba zilibana.

“Ilibidi mimi na Hermy tuingie kwenye mall tununue mic kwanza, tukanunua mic na cable na sound card tukaenda katika room ya Diamond tukaweka kwenye meza ya chakula tukarekodia hapo kwahiyo tukatengeneza studio hotelini,” AY alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.

“Kwahiyo kilichofanyika nikaandika verse pale kama leo halafu kesho tukashoot video,” aliongeza Diamond.

Wanasema walitumia takriban saa moja kumaliza kurekodi.

Video ya wimbo huo imepokelewa vizuri na hadi sasa ina zaidi ya views 170k.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents