Burudani

Utake, Usitake Salama Anaweza

Salama JabirKuna kila sababu ya kumpa credit zake Mtoto wa Kizenji, asiyejua kuyafumbia macho makosa ambayo wanaburudani wengi huyafumbia Macho lakini yeye anakupa cheupe, ucheke, unune, ukasirike, umpende, umchukie hiyo ni shauri yako, si mwingine bali Salama Mwana wa Jabir

Salama JabirKuna kila sababu ya kumpa credit zake Mtoto wa Kizenji, asiyejua kuyafumbia macho makosa ambayo wanaburudani wengi huyafumbia Macho lakini yeye anakupa cheupe, ucheke, unune, ukasirike, umpende, umchukie hiyo ni shauri yako, si mwingine bali Salama Mwana wa Jabir, mtangazaji maarufu katika kituo cha luninga cha East Africa TV channel5.

 

 

 

Wenye akili timamu hukubali kile ambacho binti huyu anakifanya kwa kuwa ni dhahiri yaonekana hafanyo kwa kuipotsha jamii bali lengo lake ni kuiweka sawa na kujaribu kupunguza dosari ambazo zipo katika engo ya burudani nchini.

 

 

 

Binti huyu anauza sura katika kipindi cha Planet Bongo ambacho kimekuwa kikijizolea umaarufu siku hadi siku kwa jinsi ambavyo yeye mwenyewe amekuwa akikiendesha kwa kuwakosoa wasanii na kuwaelekeza nini cha kufanya kuhusiana na kuzifanya kazi zao kuwa bora.

 

 

 

Wapo ambao wanakerwa sana na binti huyu kutokana na kile ambacho amekuwa akikifanya lakini cha kufurahisha waliomuelewa mpaka leo unaweza kuona mabadiliko makubwa tu katika video za wasanii wa kibongo lakini wabishi wameabki wanafanya madudu, katika hili sio siri binti anahitaji big up za kufa mtu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents