Habari

Utafiti: Tweets zinaongeza utazamwaji wa vipindi vya TV

Mvua ya tweets kuhusu kipindi cha TV huvisaidia vipindi hivyo kutazamwa zaidi, utafiti mpya umesema.

8223c18230c8561f66c23dfc31e6a9ee
Mkasi chenye followers 27,482 na zaidi hupata tweets nyingi zaidi kwa show za TV za Tanzania na ndio maana kimekuwa kipindi kinachotazamwa zaidi

Kwa mujibu wa kampuni ya uchambuzi za vyombo vya habari ya Neilsen, comments nyingi kuhusiana na kipindi fulani zinaashiria ongezeko la namba ya watazamaji.

Wakiangalia trends za dakika kwa dakika, watafiti wamegundua kuwa wingi wa tweets kuhusu kipindi zilisababisha mabadiliko makubwa ya asilimia 29 ya episodes 29 walizozichambua.

Reaction za kwenye Twitter kuhusiana na kipindi zimekuwa kipimo kizuri cha kama kipindi kimefanikiwa ama lah.

Mwezi uliopita kipindi cha Ben Elton cha BBC kiitwacho The Wright Way kilisitishwa baada ya kukosolewa vibaya kwenye Twitter.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents