Habari

Usiku wa Mtanzania

 

Lady Jay Dee, Sikinde Ngoma  , vikundi vya ngoma za asili , Ngoma  ya Ukae na Waane Star  pamoja na mwanamuziki kutoka Kenya Kidumu wanatarajia kutumbuiza katika sherehe za kuadhimisha kutimiza kwa  miaka 10 ya  Usiku wa Mtanzania , utakaofanyika katika ukumbi wa  Karamjee tarehe 3 Desemba mwaka huu  jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi  mwendeshaji wa Hoteli ya Peacock Damas Mfugale aliwaambia waandishi wa habari leo kuwa Peacock hoteli ni hoteli inayodumisha na kuendeleza mila,  desturi na utamaduni wa mtanzania , hivyo kwa kuwajali wateja wakaanzisha usiku wa mtanzania  ambapo vyakula vya asili ya Tanzania vinaandaliwa kwa ladha ya asilia.

Sherehe hii itaadhimisha  kutimiza kwa miaka 10 ya usiku wa Mtanzania ambapo  kila siku ya Jumatano huwa ni desturi ya kuwa na usiku wa mtanzania na   manthari ya hoteli hugeuka na kuwa ya asili ili kuleta maana halisi ya lengo la usiku huo.

Pia katika usiku wa Mtanzania  wa kutimiza miaka kumi Benki ya Posta, Shear Illusions, Vayle Springs, na Precision Air ni makampuni ambayo yamedhihirisha kuunga mkono mila na desturi za kitanzania.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents