Burudani

Usichokifahamu kuhusu ‘concept’ ya video mpya ya Nay wa Mitego ‘Mr Nay’

Kwa mtu ambaye tayari ameiona video mpya ya Nay Wa Mitego, ‘Mr Nay’ huenda swali la kwanza ambalo atajiuliza mara baada ya kuitazama au akipata nafasi ya kukutana na Nay atamuuliza ni ‘hiyo concept ya video, zile damu damu na ‘mask’ za kutisha, minyororo na hizo sign zote zina maana gani?’

Mara nyingi au mara zote director wa video au filamu anapokuwa anaandaa muongozo (script) hua anakuwa na story ambayo anaifuata, au lazima awe kwenye nafasi ya kuelezea maana ya ‘concept’ ya video ili mwisho wa siku mtazamaji apate mantiki ya anachokiona kwenye TV.

Nimeanza na maelezo hayo ya utangulizi ili kukuvuta katika video mpya ya Nay Wa Mitego ‘Mr Nay’ iliyotoka jana Ijumaa .Video hiyo imefanyika nchini Kenya na kuongozwa na Kevin Bosco Jnr.

Sasa ambacho hufahamu kuhusu video hiyo, Nay ndiye aliyetoa idea ya kile unachokiona kwenye video hiyo, ni mawazo yake mwenyewe ambayo aliyawasilisha kwa director na kutaka ifanyike hivyo.

Cha pili usichokifahamu ni kuwa pamoja na kuwa idea ni ya kwake lakini yeye mwenyewe Nay hajui ina maana gani, wala hajui kwanini ametaka video iwe hivyo na hajui uhusiano uliopo kati ya wimbo na concept ya video, lakini ameamua tu hiwe hivyo.

“Kitu ambacho ninakumbuka wakati tuna shoot imefika katikati ya video kuna baadhi ya vipande ambavyo vilikuwa vinahitaji zile sign flani na dizain kama ya damu ni idea zangu, director akaniuliza kwanini unataka tufanye hivi nikamwambia mi naomba ufanye hivi ufanye hivi akasema sawa tunafanya tumeshaandaa kila kitu, kwanini unapenda video iwe hivyo nikamwambia hiyo ni idea yangu sielewi kwanini nataka nitanye hivi na sijui kama tutapata kile tunachokitaka, mi napenda video yangu iwe hivi, sijui tu niliamka siku hiyo nikawa nimeota ndoto flani sijui ilikuwa ndoto sijui nini kwamba nahitaji vitu flani hivi video yangu iwe na style flani hivi.” Nay aliiambia 255, ya XXL ya Clouds FM.

Hizi ni baadhi ya comments za mashabiki kuhusu video hiyo:

godswill bosco -aaaaaah aaah he killed them aiseee,iko poa but the issue ya kumfunga nyororo mwana dadda haiko poa soon italeta utata na chama cha kutetea haki za wanawake,get ready bro Nay to xplain in details what did yu mean

JIMMY ASEKILE-video iko poa but i deal ya kumshikilia mwanamke kwa mnyololo cjaipenda aisee cjui labda me nimeelewa vipi!!!!

Jacob Erobuam – Mr.Nay Video ni nzuri, na mziki ni mzuri ila mistari bado haijakaa vizuri, mbona kwenye video yako sura ya shetani imejionyesha mara nyingi? unataka watu wamuabudu shetani?

Nay amesema video yake imefanikiwa kwenda kwenye vituo vikubwa vya kimataifa kitu ambacho hakukitegemea.

Kuhusu gharama za video, “Video haijanicost hela nyingi sana, imenicost kama milioni sita saba hivi”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents