Bongo5 Makala

Usichokifahamu kuhusiana na jinsi video ya ‘Imebaki Story’ ya Hemedy PHD ilivyotengenezwa

Umeitazama video ya wimbo mpya wa Hemedy PHD? Wimbo wake ‘Imebaki Story’ ni nzuri sana na kinachofurahisha zaidi imefanywa na waongozaji wa video wa Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=m9p1Y6QHSDY&spfreload=10

Video hii imefanywa na kampuni ya Kwetu Studios na kuhaririwa na muongozaji mkongwe wa video, Adam Juma.

Ukitaka kuuonesha uzuri wa Tanzania kwa mataifa ya nje, sidhani kama maghorofa au vitu vilivyotengenezwa na binadamu ni vitu watakavyovishangaa. Uzuri wa maliasili za nchi yetu ni kitu pekee kinachoweza kuonesha utofauti wa video ya Chris Brown na ya msanii wa Tanzania.

Imebaki Story inakuonesha mandhari ya kuvutia sana kuanzia kwenye picha zinazomuonesha akiwa kwenye boti ndani ya ziwa lililozungukwa na misitu ya kuvutia. Ziwa hilo linaitwa Duluti na lipo mkoani Arusha.

“Hili ni ziwa ambalo lina space kubwa, sio sana lakini ni kubwa kwa kiasi chake kama lilivyoonekana,” Hemedy ameiambia Bongo5.
“Nilikuwa nauoga sana wa kuingia kwenye kile kiboti kilikuwa ni kidogo na isitoshe kilikuwa ni cha kusukuma kwa ile miiko ya pembeni. Nikajaribu kuuliza kuna urefu gani pale wakaniambia ni mita nne yaani ni viwanja vya mpira vinne kwenda chini,” anasema.

“Nilikuwa muoga na nilichukua risk kwasababu nilikuwa nataka kitu kizuri, mwisho wa siku nikajaribu na nikaweza kwasababu ilinibidi nisogee mpaka katikati ya ziwa ili jamaa waanze kurusha helikopta (drone) ili tupate shots. Kwahiyo nilikuwa muoga sana na baada ya kumaliza kushoot nilipiga kelele sana kuomba jamaa aogelee aje anifuate anivute sababu sikuwa kwenye situation nzuri, nilikuwa kwenye pressure ya hali ya juu.”

Hemedy anasema walienda kwenye ziwa hilo kushoot kipande cha kuanzisha video (establishing shot) lakini baada ya kupata picha ya kuvutia sana, waligundua kuwa inabidi Hemedy aingie ndani ya boti ili kuwafanya watu waamini kuwa ni shot halisi na sio shot ya kudownload tu.

Katika kutafuta upekee wa video hiyo, Hemedy amesema wazo la kwanza la kuitengeneza lilibadilika.

“Na ndio maana ukiangalia video unaona mwanamke tumemficha sura. Lengo letu ni kuonesha kwamba huyu mtu hayupo tena kwenye maisha imebaki story. Kuna parts zinaonesha jinsi gani namfuata mwanamke lakini siwezi kumsogelea, hiyo inaonesha kuwa hayuko tena na mimi. Yuko library anapita anasoma vitabu, nilipo na yeye alipo ni vitu viwili tofauti ni kama tuko kwenye ulimwengu tofauti,” amesema.

Hemedy anasema hakupenda kufanya video zilizoeleka za chumbani, sebuleni au kwenye nyumba ndio maana alitaka kufanya kitu tofauti kwa kwenda kwenye mikoa mingine.

Anasema changamoto za kufanikisha kutengeneza video hiyo zilikuwa nyingi ikiwa ni pamoja na kuwapata wazungu hao wawili wanaonekana ambao hiyo ilikuwa ni video yao ya kwanza kufanya katika maisha yao na walikuwa na ugeni mkubwa wa camera.

Changamoto nyingine ilikuwa ni kupata location hizo ambazo nyingi zilikuwa za mbali na zingine zilihitaji vibali. Hiyo ilimpa Hemedy kazi ya ziada kwakuwa mambo yote ilibidi ayafuatilie mwenyewe na hivyo kumchosha kwa kiasi kikubwa.

“Nguo nadesign mwenyewe, kila kitu najivalisha mwenyewe, make up najifanyia mwenyewe kwahiyo nilikuwa kwenye mazingira ya mtu ambaye hajatulia,” amesema Hemedy.

Video hiyo imemgharimu Hemedy shilingi milioni 15 na anaamini kuwa itaitangaza Tanzania pamoja na yeye mwenye kumfikisha mbali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents