Habari

Usiambatane au kuongozana na walioshindwa, watakukatisha tamaa

Watu hawa wawe ni ndugu, marafiki au majirani kama wameshindwa usiendelee kusikiliza kushindwa kwao bali angalia wewe au hakikisha hauingii kwenye vitu ambavyo wao wameshindwa. Kuna usemi unasema “ndege wenye mabawa ya aina moja huruka pamoja kama sijakosea”. Huwezi ukaongozana na mtu ambaye hamna ajenda moja huko ni kupoteza mwelekeo hata kama huyo mtu ni rafiki yako ambaye mmeshibana.

man-with-friends

Watu walioshindwa na kukata tamaa wanaamini vitu haviwezekani kwasababu wao wameshindwa au hawakuwa makini hivyo wanataka uamini hivyo. Kaa mbali nao, kushindwa kwao sio kwako kwani kila mtu amepewa uwezo tofauti wa kufanya na kufikia matarajio yake katika maisha.

Ukikata tamaa ni mwanzo wa kupoteza mwelekeo wa maisha au biashara yako. Ninapozungumzia walioshindwa ninazungumzia watu ambao wamepoteza mwelekeo na hawawezi kutoka hapo walipo kuelekea mbele, hivyo ndani ya mawazo yao kumejaa uchungu, kushindwa na kukata tamaa au kukosa matumaini kama wanaweza kuinuka tena. Hao ni watu hatari wakikuzunguka kila siku ya maisha yako wanakuambukiza kitu ambacho kitakufikisha pale walipofika.

Unahitaji kijichunguza ni nani anayekuzunguka kila siku au unatumia muda wako na watu gani kila siku? je mwelekeo wao kimaisha na kibiashara ukoje? Je ni watu ambao unaweza kupata ushauri kwao?

Faida ya kukaa na watu wenye mwelekeo, wanakupa tumaini kwamba unaweza kufikia malengo yako tokea hapo ulipo. Kushindwa ni sehemu ya kufikia mafaniko usipokaa pale pale uliposhindwa, unahitaji kuinuka na kufikiri kwa namna ya tofauti kufikia kule unakotakiwa kufika. Unahitaji watu sahihi, wenye moyo wa kujifunza na kunuia kufanya vizuri au kuboresha pale ambapo wamefika sasa.

Unahitaji watu ambao wanajua kushindwa ni nini na waliinuka kutoka sehemu walioshindwa wakafanya vitu vikubwa. Namna walivyopita wao sio lazima na wewe upitie bali unahitaji kujifunza ili ufikie malengo yako.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents