Burudani

Ushirikiano wa ma-producer wa Tanzania upo kwa asilimia ndogo sana – Nahreel

Ili muziki wa Tanzania ukue na uende mbali inahitajika nguvu ya pamoja upande wa wasanii na hata watayarishaji wa muziki.

Nahreel

Producer Nahreel wa The Industry amesema kuwa upande wa watayarishaji wa muziki ushirikiano uliopo ni mdogo sana.

“Ushirikiano wa maproducer wa Tanzania kufanya kazi pamoja haupo kwa asilimia kubwa ni maproducer wachache sana ambao wanakuwa na ushirikiano” Nahreel ameiambia Bongo5.

Nahreel ambaye mwaka huu ameproduce kazi nyingi zilizofanikiwa kushika chati kwenye vituo mbalimbali vya nje ikiwemo Nigeria, amegusia tatizo linalofanya watayarishaji wa Bongo kushindwa kushirikiana.

“Hii inatokana tu kwasababu mimi nadhani ile kuwa insecure. Maproducer wengi wanaona kama wakishirikiana wanapoteza nguvu ya kuonekana amefanya ile kazi, lakini mimi nadhani lengo la kutayarisha muziki ni kutengeneza muziki mzuri bila kujali mmetengeneza watu wangapi.”

Kwa upande wake amesema producer ambaye wanaelewana zaidi na ambaye amekuwa akishirikiana naye katika kazi zake nyingi ni Chizan Brain.

“Mimi kama mimi kazi zangu nyingine nakuwa nashirikiana na maproducer wengine, kwa mfano producer kama Chizan Brain nimekuwa nikishirikiana naye kwenye nyimbo nyingi ambazo tumeanza kufanya katika studio nyingine hadi sasa hivi nipo The Industry.” Alimaliza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents