Burudani

Ushauri wa Dully Sykes aliowapa watangazaji wa Kenya: Msipige nyimbo za wa-Nigeria, ni wezi namba 1 duniani (Audio)

Mwana FA alishawahi kutamka kuwa haupendi muziki wa Nigeria na kutoa sababu zake (Ingia hapa), na Dully Sykes naye hivi karibuni ametoa kauli kama hiyo alipowashauri watangazaji wa radio za Kenya waache kupromote muziki wa Naija na badala yake watoe nafasi zaidi kwa wasanii wao wa Kenya.

Dully pilipili
Dully akiwa kwenye studio za Pilipili FM, Mombasa

Dully ametoa kauli hizo alipofanyiwa mahojiano na Chris na Chigulu kupitia Pilipili Fm ya Mombasa, Kenya.

“Nyinyi ma presenter nyinyi ndo mbadilike,” alisema Dully. “Watengenezeni wanamuziki wenu, nyinyi mtakapoanza kupiga nyimbo za wasanii wa nje mwisho wa siku jamaa wanakosa soko sasa wanaona bora waige kule ili nyie mpige. Kwanini sasa nyinyi mnaweza kupiga nyimbo za watu wa nje masaa manne halafu mnapiga nyimbo za wa hapa robo saa tu.

Kwani muziki wa Nigeria waliutafuta kwenye google? Si waliusikiliza na ndio maana wana u-request, na wana request wapi, kwa radio, si wangeenda ku-request google kwasababu ndio walikoupatia. Nyinyi ndio mnauwa muziki, kwahiyo nyinyi pendekezeni muziki wa kwenu ili wanigeria wasipate nafasi.”

Dully aliendelea,

“Mnigeria si mtu mzuri, mnigeria ni mwizi namba moja Afrika, Mnigeria kila sehemu yupo unajua, Mnigeria South Afrika kama nchi yake, mnigeria huko ulaya huko ndio wametawala wao, ni wezi namba moja duniani, kwahiyo anauwezo wa kumteka mtu hata kwa uchawi, cha maana ni hivi tuuwe Unigeria turudi kama zamani.

Nyinyi msipige nyimbo za hawa wanigeria, wezi tu hawa wanakuja wanachukua tu hela huku, mtu anakuja hapa anachukua milioni 5 ya Kenya, milioni 5 ya Kenya anaitumia Kenya? Hatumii Kenya anaenda kutumia kwao uchumi wa nchi yake unakuwa.”

Msikilize hapa Dully akiongea mwenyewe
http://youtu.be/eqqizDe4_sM

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents