Burudani

Urafiki wa AY na Hermy B warejea kwa kasi (Picha)

Hakuna anayeweza kuisahau chemistry ya Hermy B na AY miaka kadhaa iliyopita. Urafiki wao ulisaidia kutengenezwa kwa hits kama Habari Ndio Hiyo, Kings and Queens, Leo na zingine kibao.

11325695_1463159683993130_2127758765_n
AY na Hermy B wakiwa jukwaani Masasi

Hata hivyo masuala binafsi na biashara yalitengeneza tofauti kati yao zilizodumu kwa miaka takriban miwili ikiwa pamoja na kuacha kufanya kazi. Licha ya kuacha kufanya kazi pamoja urafiki wao ulirejea taratibu na sasa mambo yanaonekana kurudi kama awali.

11950480_1013172172067070_1560996234_n
AY akiwa na Hermy B na Fid Q Mtwara. Walipokaa ni nyumba ambayo AY alizaliwa

Wiki iliyopita AY alishare picha akiwa studio na Hermy B na Marco Chali na kueleza kuwa anarekodi ngoma mpya na watayarishaji hao.

11252465_1647628742120195_616091842_n

Hivi karibuni pia AY ambaye yupo kwenye Zigo Tour alimchukua Hermy na kwenda naye hadi Mtwara na Masasi ambako pia walipanda jukwaani pamoja.

Hakuna shaka kuwa wawili hao watakuja na kazi kali zaidi hivi karibuni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents