URA Yaiadhibu Mtibwa Tusker

TIMU ya Mtibwa Sugar imeanza vibaya michuano ya Kombe la Tusker kwa kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Mamlaka ya Mapato Uganda (URA).

TIMU ya Mtibwa Sugar imeanza vibaya michuano ya Kombe la Tusker kwa kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Mamlaka ya Mapato Uganda (URA).
Mchezaji Tony Mwawejie alifunga bao la kwanza katika michuano ya Tusker mwaka huu katika dakika ya 55 kwa shuti lilomshindi kipa wa Mtibwa, Shaaban Kado.
Kipa huyo wa Mtibwa Sugar, ndiye aliyekuwa kikwazo kwa URA kupata ushindi wa mapema katika kipindi cha kwanza.
Katika dakika ya 14 na 19, washambuliaji wa URA, Ismail Kigol na Martin Muwanga mashuti yao yalipanguliwa na kipa Kado aliyekuwa kikwazo kikubwa kwao.
Hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika hakuna liyefanikiwa kuziona nyavu za mwenzake huku mpira ukichezwa kwa sehemu kubwa kwenye nafasi ya kiungo.
Kocha wa URA, Moses Basena alisema timu yake imecheza vizuri lakini wameshindwa kutumia nafasi walizopata na kupata ushindi mkubwa zaidi.
Mwenzake wa Mtibwa, Salum Mayanga alisema timu yake haikucheza vizuri kutokana na wachezaji wake kutokaa pamoja kwa muda mrefu ndiko kulikochangia matokeo hayo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents