Habari

Upo kwenye ofisi ambayo bosi wako hakupendi? Fanya haya

Si kitu cha kawaida mfanyakazi na bosi kuwa na mawazo tofauti au kwenda mwelekeo tofauti kuhusu mahusiano yao. Kwa bosi ambaye anafikiri anaheshimika na kila mtu anaweza kuchukuliwa kana kwamba ni mtu mtemi kwa wale ambao anawaongoza na vile vile unaweza kushangaa pia bosi ambaye unasema anakupenda au una mahusiano naye mazuri kwa wengine haheshimiki hivyo na hathaminiwi pia.

Frustrated businessman with laptop computer

Mara nyingi hatujui namna ya kuhukumu kwa namna tunavyowaangalia watu wengine. Kwakuwa watu ambao tunaweza kuonyesha pole na kicheko kwa nje bali ndani yetu kuna hasira kali, dharau pamoja na kuficha hayo yote mtizamo wa tofauti pia unaruhusiwa kwenye mahusiano hayo.

Cha kushangaza, kupata hizo hisia na kwa uwazi zaidi kunaweza kuwa na msaada mkubwa kwa bosi na mfanyakazi mwenyewe kwa namna ambavyo wanahusiana .

Watafiti wa mambo ya mahusiano kazini wamegundua kuwa panapokuwa na mawazo tofauti na vile ambavyo kila mmoja anayatizama mahusiano hayo ufanisi wa kazi huathirika pia. Hamasa ya kazi inapungua inapoonekana kuna mtizamo tofauti kati yao, na hali hiyo haibadiliki endapo mfanyakazi anaona mahusiano yako vizuri kuliko hali ya bosi ilivyo kwa mtizamo wake.

Vile vile hamasa ya kazi ilionekana kuwa kubwa pale ambapo bosi na mfanyakazi wana uwezo wa kuangaliana uso kwa uso katika mazungumzo yao hata kama mahusiano yao ni mabaya mfanyakazi inampa hali ya kufanya kazi zaidi. Ingawa wengine wanadhani ni vizuri kuonyesha hali kana kwamba unampenda bosi wako au kuonyesha kwamba hakuna tatizo kati yenu lakini tabasamu la kuigiza lina madhara makubwa na kuleta matokeo mabaya, ni bora mtu ajue kuwa hamuendani lakini kazi itafanyika kwa heshimiana vizuri.

Unatakiwa kuwa na mazungumzo ya upole na utaratibu hata kama hamuwezi kutizamana usoni ila mnaweza kusafisha hali ya hewa iliyopo. Unaweza kusema kitu kama vile ” Ninajua huwa hatuwezi kukubaliana kwenye mambo mengi na namna kazi inavyotakiwa kufanyika” au ninajua tuna hulka na mtizamo tofauti katika mambo bali ninapenda tukubaliane na jambo hili kwa pamoja.

Kama unashindwa kusema au unajifanya hutaki kujali kuhusu bosi wako, hauko peke yako, kukubaliana kwamba unamchukia au hamuendani inawezekana kikawa kitu cha ajabu. Vile vile ni vibaya au kudhani kila mtu unaweza kuendana naye lazima tukubaliane kuwa kuna mahali tutakwaruzana au kushindwa kuelewena kwa namna moja ama nyingine lakini si vibaya inapotokea hivyo.

Kama hujisikii vizuri au unaona kama watu hawakupendi, unaweza kutumia mawazo haya machache yaweze kukusaidia;

Usichanganye wale ambao hufanya vitu ili wapendwe, unapotaka kila mtu akupende inasababisha wewe kuwa na hali ya kufurahisha watu. Na hii husababisha watu wengine kuacha vitu vya msingi na utu wao au heshima yao kwa ajili ya watu wengine ili kufanya vitu fulani wapendwe zaidi. Kitendo cha wewe kufurahisha kila mtu si lazima kwamba kila mtu atakupenda lakini kinapunguza hali ya wewe kuridhika katika maisha yako.

Simamia mawazo yako ya msingi hata kama watu wengine wanaona ni hasi au kinyume na vile wanavyotaka. Unaweza kufikiri labda bosi wako hakupendi hivyo hutafanikiwa, hiyo si kweli haujafungwa kwa mtu yeyote. Kubaliana na hali kwamba hujisikii vizuri kama watu hawakupendi, lakini hisia hizo haziwezi kukuua. Kitu kingine unachotakiwa kujua ni kwamba unapokutana na hali hiyo mara nyingi inakujengea ujasiri wa kuweza kupambana na hali hiyo wakati mwingine na kukujengea ujasiri kihisia.

Jifunze kuwa halisi na ujifunze kuwaheshimu watu wengine na kuwahudumia vizuri. Onyesha kupongeza panapostahili pasipo stahili usimpongeze mtu au kumpa pongezi za kinafiki. Onyesha mawazo na mtizamo wako. Miliki hisia zako na kukubaliana kwamba yupo tembo ndani ya chumba na unaweza kuboresha jambo hilo. Hulazimiki kumpenda bosi wako na bosi wako halazimiki kukupenda ili kujenga timu nzuri, ila kuna vitu mnaweza kukubaliana na vikafanyika.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents