Burudani

Uongozi wa jarida la Baabkubwa wajitolea 1.2m kuchangia matibabu ya Jetman

Baada ya dhiki ni faraja. Uongozi wa jarida la Baabkubwa umejitolea kumchangia msanii na mtayarishaji wa muziki nchini Jetman ambaye amekuwa kitandani kwa takriban miaka mitano kutokana na tatizo la kupooza mgongo kiasi cha shilingi milioni mbili na laki mbili.


Kulia ni bosi wa Baabkubwa, Joe Kariuki akimkabidhi Lilian Masuka mchango wao matibabu ya Jetman

Uongozi huo umejitoa mchango huo huku wakijitolea kununua beat moja lililotengenezwa na Jetman pamoja na baadhi ya wasanii wakiongozwa na Mrisho Mpoto, Msami na wengine waliohudhuria katika uzinduzi wa jarida hilo ambalo lilikuwa kimya kwa takriban miaka miwili.

Bosi wa Baabkubwa ambaye ni Mkenya, Joe Kariuki amesema mbali na mchango huo atajipanga pamoja na wafanyakazi wake ili waweze kuangalia uwezekano wa kwenda kumtembelea msanii huyo nyumbani kwao jijini Mwanza.

Shilingi milioni 12 zinahitajika ili aende India kupata matibabu. Tunaweza kuungana naye kwa kutengeneza nyimbo kwa kutumia riddim yake na kutoa mchango wa fedha za matibabu.
Wewe unaweza kuchangia kupitia 0757 62 62 07. Jina ni GODFREY KUSOLWA.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents