Habari

Unywaji pombe kupita kiasi ni hatari kwa ndoa iwapo mmoja wa wanandoa si mnywaji

Watafiti wa mambo ya mazoea katika vinjwaji na madawa ya kulevya baada ya utafiti wa muda mrefu wamegundua kuwa ndoa nyingi zenye matatizo hasa ya unywaji pombe kupita kiasi inategemea sana na wanandoa kama wote wanakunywa kupita kiasi au ni mmoja wao ndio mnywaji kupita kiasi.

City Wine Tour_couple in window

Kutokana na utafiti uliofanya na chuo kikuu cha Buffalo Research Institute on Addictions (RIA) kwa wanandoa 634 kutoka wakati walipooana wakagundua kuwa ndoa ambazo mwenza mmoja ni mlevi kupindukia wana hatari ya kuachana kwa kiasi kikubwa kuliko wote wakiwa walevi wa kupindukia.

Kama wote ni walevi wa kupindukia, talaka zilikuwa sawa tu na wale ambao si walevi kabisa. matokeo yao yanaonyesha kuwa tofauti kati ya wanandoa ambao ni walevi ni tabia ukiondoa ulevi wenyewe. Kitu ambacho hutokea ni kushindwa kutimiziana haja ya tendo la ndoa, kuachana pamoja na talaka anasema Kenneth Leonard mkurugenzi na mwandishi wa utafiti huo.

Kutokana na utafiti wao inaonyesha kuwa wanandoa ambao mmoja wao ni mlevi wana hatari ya kuachana kwa asilimia kubwa zaidi kuliko wote wakiwa walevi. Hiyo inatokana na kwamba je ni kitu gani kinachowaunganisha hao wanandoa.

Mlevi mmoja aliyebahatika kuachana na tabia hiyo anasema hivi “Unywaji wa pombe kupita kiasi unasababisha kuvunja mahusiano mengi, ingawa wanywaji wengi wanafikiri wakishakunywa pombe ndipo wanaweza kuongea vizuri na kuhusiana vizuri na watu wengine. Ukweli wa mambo ni kwamba unapokunywa habari nyingi ni kuongelea ni utakunywa ngapi na kuongea vitu vingi ambavyo huwezi kuongea au kuvifanya ukiwa kwenye akili ya kawaida”. Wengi wa wanywaji hao ndio hufanya familia zao kuharibika kwa kuwa hakuna uhusiano mzuri kati yao na watoto hivyo kusababisha unyanyasaji wa kijinsia, ugomvi ndani ya nyumba hata na familia yenyewe kukosa mwelekeo.

Vile vile anasema ya kuwa wanywaji wengi ni wabinafsi kwani unapokuwa umelewa kila kitu unawaza ni namna ya kujinufaisha wewe kihisia, hivyo inakuwa ngumu kufikiria kuhusu mke au mume na watoto. Hivyo unawaacha watoto na familia katika mazingira magumu ya kukosa mzazi wakati mzazi huyo yupo ila ametekwa na pombe kupita kiasi.

Mtu huyo anaendelea kusema  baada ya kuacha kuwa mrevi amerudisha imani kwa rafiki zake na familia yake, ameweka kuwa baba ambaye analea watoto wake na familia yake, hicho ni kitu amabacho alikuwa hawezi kufanya wakati alipokuwa mlevi. Hivyo amewaasa wanywaji kupita kiasi kwamba si rafiki zako wanaoweza kuamua wewe unataka kuwa nani ila ni wewe mwenyewe unaweza kubadirisha mazingira yako na kuweza kufanya jambo sahihi na kuwa mtu mahili ambaye unatakiwa kuwa. Mabadiriko yanaanza kwako na si kwa mtu mwingine.

Unywaji pombe kupita kiasi ni hatari kwa maisha yako na kizazi chako, chukua hatua.

 

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents