Michezo

Undani wa jinsi Floyd ‘Money’ Mayweather anavyotumia hela zake, hutaamini..

Mbele ya pambano lake la September 14 ambapo atalipwa dola milioni 41.5, bondia ambaye hajawahi kushindwa, Floyd Mayweather amekuwa akiishi maisha ya kuchezea sana fedha.

article-2413437-1BA58FED000005DC-635_306x423

Bondia huyo mwenye miaka 36, anayetambulika kama bondia bora zaidi duniani leo, amepewa jina la utani ‘Money’ na kwa kutazama picha ambazo huzipost mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii si kazi ngumu kubashiri kwanini aitwe hivyo.

article-2413437-1BA58FFD000005DC-289_634x440

Mara nyingi Mayweather amekuwa akipigwa picha akionesha lundo la hela na hana aibu katika kuzitumia pia.

Bondia huyo anapenda kulipa kwa cash katika vitu vingi na mara nyingi mmoja wa wapambe wake hubeba begi lenye noti za dola mia mia. Utumiaji wake wa fedha ni mkubwa kiasi ambacho husisitiza katika kuvaa sneakers (viatu) mara moja tu kabla ya kuondoka hotelini.

Pia huvaa boxer zake mara moja kabla ya kuzitupa, yaani kila siku huvaa boxer mpya na harudii.

Magari ni vitu vingine anavyotumia hela nyingi na pia ana seti mbili za magari ya kifahari yanayofanana na yenye rangi maalum ili kumsaidia akumbuke yupo kwenye jiji gani.

article-2413437-1BA58D9B000005DC-769_634x419

Floyd_Mayweather_Rolls_Royce_Coupe_Rolls_Royce_Phantom

Kama gari ni jeupe basi yupo Las Vegas, kama gari ni jeusi basi atakuwa jijini Miami.

Timu ya wapambe wake imepewa jina ‘The Money Team,’ ambalo hulitumia pia kwenye biashara zake. Akiwa kwenye ziara ya kupromote pambalo lake lijalo na Saul ‘Canelo’ Alvarez, Floyd alimuonesha karatasi ya benki mwandishi wa ESPN, Tim Keown ilioneshwa kuwa na jumla ya dola milioni 123 na kumwambia ‘One account, baby.’

Wakati wa ziara yake kwenye majiji 11, Mayweather alikuwa akisafiri na ndege binafsi lakini walinzi wake wanne aliwakodia ndege yao binafsi pia. Kwenye ndege yake anasafiri na kinyozi wake binafsi japo mara nyingi huwa na kipara.

Akiwa jijini New York, bondia huyo alitumia karibu dola robo milioni kwa kununua heleni na mikufu ya binti yake mwenye miaka 13, Iyanna. Wapambe wake wa Team Money ambao ni kama 20 hivi hutumia muda mwingi kusubiri Mayweather aamue nini cha kufanya baadaye.

‘Hatujui tunachokifanya hadi tukifanye,” alisema mmoja wa wasaidizi wake. Unazoea tu.

Ukiwa na hela nyingi ni lazima uwe na msichana mrembo pia sio? Kama alivyo mpenzi wake, Shantel Jackson.

Shantel-Jackson-16

ShantelJackson42

Shantel-Jackson-pool

tumblr_lrszwh7tam1qbc14wo1_500

tumblr_mcfmqqmKcX1qd35plo1_500

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents