Habari

Unatamani kuajiriwa mwaka huu? Unahitaji ubongo wa ziada

Ujumbe kwa wanafunzi walioko vyuoni na wanategemea wakimaliza wapate kazi. Mawazo yao ni sahihi ila kwa mwaka huu na kuendelea, mambo yanazidi kuwa magumu. Mambo yataendelea kuwa magumu kwasababu tumeongeza vyuo na wanafuzi wanaohitimu kila mwaka ni wengi kuliko kazi zilizopo. Hebu jiulize kwanini upate kazi wewe amabye utamaliza chuo mwaka huu wakati kuna watu wanasota tokea wamehitimu na kazi hazijapatikana?

Fikiria utaingiaje huku mtaani? Je una jambo gani llitakalo fanya wewe uweze kupataka kazi na mwingine akose? Wakati huu unahitaji ubongo wa ziada, jaribu kufikiri kwa upande mwingine, achana na fikra ya kwamba kazi zipo na zinakusubiri. Kama wewe unategemea kazi za serikali, endelea kusubiri ila kama unategema sekta binafsi unahitaji kazi ya ziada. Unahitaji kuwashawishi kama kweli hiyo kazi wanatakiwa kukupa wewe. Je unawashawishi vipi?

Cheti unacho, Je ujuzi unao? Una ujuzi gani uliopata hapo chuoni, kitu gani kinakutofautisha na watu wengine uliosoma nao? Hapa sio GPA, ninazungumzia kama wewe umesomea uandishi wa habari onesha habari ulizoandika mpaka sasa zina weledi kiasi gani na mtu akisoma unapata maoni gani? Kama umesoma mambo ya teknolojia , umefanya nini au bidhaa gani umeshatengeneza ambayo itawashawishi wakuone unaweza kufanya kazi.

Unajua kuongea? Ninapozungumzia kuongea ninazungumzia namna unavyozungumza na watu vilevile kujieleza mbele za watu.Je unajua kuongea Kiingereza vizuri na kukiandika. Je unaweza kuwasilisha kitu kwa ufasaha na watu wakaelewa? Usidanganyike na watu wanaosema uzalendo ni kuongea Kiswahili, katika katiba ya nchi hii Kiingereza ni lugha rasmi hivyo huwezi kuikwepa na vilevile inakuongezea mwanya wa kuwasiliana na watu mbalimbali ndani ya nchi na nje ya nchi. Sisi kama watanzania hatujafikia uwezo wa kuongea Kiswahili tu halafu mambo yaende, bado ni tegemezi. Usiseme mbona wachina wanaongea lugha yao, mbona wafaransa n.k  wote hao kiuchumi na teknoloJia wanajiweza na kujitegemea. Bila kupoteza muda jifunze kuongea Kiingereza vizuri na hata unapoongea mbele za watu uwe na ujasiri.

Kama una wazo la biashara anza kulifanyia kazi kidogo kidogo. Wakati tulionao ni teknolojia na mawasiliano vinafanya kazi kwa nguvu na kasi kubwa, hakikisha unavitumia katika biashara zako. Usifikiri kizamani zamani, utapoteza wateja na utashindwa kama wengine walivyoshindwa.

Achana na makundi yasiyokuwa na mwelekeo. Maisha ni ya kwako, hivyo unahitaji kufanya vitu kwa kuangalia unakokwenda na sio wanaokuzunguka. Baada ya chuo utabaki peke yako,uwe na akili timamu na ufanye kazi au project zako mwenyewe acha kuigilizia maisha huwezi kuiga.

 

 

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents