Burudani

Unataka kuacha kazi? Soma hapa kwanza kabla hujaamua

Inawezekana una sababu za kutosha za kukusababishia ufanye maamuzi ya kuacha kazi, kabla ya kufanya maamuzi hayo soma mambo yafuatayo halafu ufanye maamuzi.

woman_sandhira_13932400488610

1. Kazi uliyonayo inaweza kukusaidia kupata kazi ile unayoipenda maishani mwako.
Unaweza kushangaa hii itakusaidiaje? Kuendelea kufanya kazi usiyoipenda  wakati mwingine inakusaidia kupata kazi unayoipenda, hii inamaanisha baadhi ya majukumu uliyonayo ni ya ile kazi ambayo unapenda kufanya. Kama hujui kwa kwenda ni ngumu kujua utafikaje huko, ila unaweza kutumia ulichonacho kufika kule unataka kufika. Hivyo usiache kazi kabla ya kupata kazi au huna kitu cha kufanya.

2. Inakusaidia kulipa gharama za maisha

Hiki ni kitu cha msingi kwa watu wengi labda kama wewe kifedha umestawi. Kazi uliyonayo ni sehemu tu ya malengo yako mafupi, pale unapojua malengo yako ya muda mrefu ndipo unapogundua kazi uliyonayo inatakiwa kulipia gharama za maisha kama  maji, umeme, chakula usafiri n.k Mpaka pale utakapojipanga kufanya maamuzi ya muda mrefu.

3. Kazi uliyonayo, je Inakukutanisha na watu na kukupa fursa za kufahamiana na watu wengine kwenye taaluma?

Kama upo tu nyumbani ni vigumu kukutana na watu na kuweza kujua fursa zinazoendelea hapa mjini. Badala ya kulalamikia mazingira ya kazi na mambo kibao tafuta fursa kwa wafanyakazi wenzako kwenye hilo shirika au wale mnaokutana nao kwenye mikutano na vikao kwa namna moja ama nyingine utajikuta unapatiwa fursa ya kukutoa hapo ulipo.

4. Kazi uliyonayo itakupa rejea nzuri

Je una mambo wa kuweka kazi uliyonayo kama rejea ya wakati unatafuta kazi nyingine? Watakapouliza uzoefu wako lazima utawaonyesha mashirika uliyofanya nato kazi hivyo chunga sana usije kuharibu hapo ulipo. Hakikisha unaondoka na nina lako ni safi wala halina vitu vitakavyoweza kukuharibia huko mbeleni.

5. Kazi uliyonayo inakupa mwelekeo wa siku yako

Upende usipende sisi watu wazima tunatumia 1/3 ya maisha yetu tukifanya kazi. Ukikosa mwelekeo wa kufanya mambo au mambo ulilozoea kila siku unaishia kupata msongo wa mawazo na matatizo kwenye mahusiano na watu wengine. Utakuwa unakatishwa tamaa unapotuma maombi ya kazi halafu hakuna majibu, unaanza kuchanganyikiwa na kukosa raha.

6. Kazi uliyonayo inashikilia utu na heshima yako

Kazi pia inakupa nafasi ya utu na kuheshimika. Watu wengi hujulikana kwa kazi wanazofanya, labda mimi ni mwanasheria, daktari, fundi, mfanyabiashara n.k changamoto huwa kubwa pale ambapo hujulikani unafanya mini, hata ujasiri wako kwa watu wengine unapungua kwa kiasi kikubwa.

7. kazi uliyonayo inakusaidia kujua vitu unavyovipenda na usivyovipenda

Unapoendelea na siku yako hebu tilia maanani kila kitu kinachoendelea kazini na watu wanaokuzunguka, utagundua vitu unavyovipenda kwa watu na usivyovipenda pia. Hii inakupa picha ya wapi na nini kifanyike, ili utakapopata kazi mpya au kupanda cheo utakuwa na uwezo wa kujua mabo mengi na namna ya kuyatatua.

8. Kazi uliyonayo inakupa faida za baadaye

Je inakurudishia gharama za elimu ukitaka kujiendeleza? Je unapata fursa ya kuhudhuria semina zenye tija ambazo zinakuongezea uzoefu? Hebu jaribu kuangalia mtu anayekuvutia na kukupa hamasa ya kufanya kazi, kama ni bosi au mfanyakazi mwenzako au hata kampuni ili uweze kujua ni vitu gani vinakufanya kuchukia hiyo kazi? je ni bosi, au wafanyakazi wenzako, au ni kampuni lenyewe au hakuna maslahi unayoyataka?

9. Kazi uliyonayo ni shetani unayemjua

Ni kweli waswahili wanasema shetani unayemjua ni heri kuliko yule usiyemjua. Haitokei mara zote, unapofanya makosa ya kuacha kazi kabla ya kupata kazi nyingine unaweza kuchukua muda mrefu bila kupata kazi. Na hiyo inaweza kukusumbua sana huku ukijilaumu.

Jipange na ujiangalie maisha yako ya mbele unataka mini? na utafanya maamuzi ya msingi na yenye kuleta tija kwako na kwa familia yako.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents