Burudani

‘Unafanya kazi na mkata viuno’ – Mashabiki wamchana Roma kurekodi wimbo na Bob Junior

Inaonekana mashabiki wa Roma Mkatoliki hawajaafikiana na uamuzi wake wa kurekodi wimbo na Rais wa Masharobaro, Bob Junior.

10513448_10152495923729962_185952916642622027_n

Roma ameiambia Bongo5 kuwa kwa miaka saba amekuwa akifanya muziki wake bila matatizo lakini kitendo cha kurekodi wimbo na Bob Junior kimegeuka kero kwa wengine.

“Baada ya kusema nafanya kazi na Bob Junior kuna kitu ambacho kimetengenezeka katika vichwa vya watu,” amesema Roma. “Kufanya kazi na Bob Junior kumekuwa na matokeo mabaya eti ‘umefanya kazi na mpaka poda, umefanya kazi na mkata viuno, umefanya muziki kwa miaka saba unafanya muziki na mpaka lips stick, yaani na wewe unaanza kukata viuno;! Hawa mashabiki wanachanganya wakati wao ndo wanasema ‘Roma kila siku unaimba kitu kile kile unatakiwa ubadilishe hata ladha’. Kwahiyo watu wameanza kuikataa nyimbo kabla hata hawajaiona. Mimi naona kinachotakiwa ni kuwaelimisha kwa sababu wengi wao hawafuatilii muziki na hawaulewi ambapo nimetokana ndio maana nikawapa mfano Kalapina alishawahi kuimba na Q Chillah na ngoma ikafanya vizuri sisi ni wasanii kushirikiana na kufanya muziki ni sehemu ya maisha yetu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents