Burudani

Ulikuwa ni mtihani kufanya video na Avril – Ommy Dimpoz (Audio)

Kwa mujibu wa Ommy Dimpoz, haikuwa rahisi kufanya video na Avril aliyemshirikisha kwenye wimbo wake ‘Hello Baby’.

Ommy ameiambia Bongo5 kuwa Avril ni msichana ambaye si rahisi macho ya mwanaume kamili kushindwa kushawishiwa na urembo wake.

“Ilikuwa mtihani kidogo unajua kufanya kazi na msichana mrembo ushawishi unakuwa mwingi. Kwahiyo nilikuwa najizuiazuia,” amesema Ommy.

“Kwasababu kwenye video kuna mambo mengi, mtu anaweza akatokea akabidilisha nguo mbele yako, kwahiyo yote niliyavumilia, ni lazima uvumilie majaribu ili kazi iende,” ameongeza Dimpoz.

Hata hivyo muimbaji huyo amesema kutokana na picha walizokuwa wanaweka Instagram, mwanzoni mchumba wake na Avril hakuelewa na hivyo kusababisha matatizo kidogo.

“Japo alikuwa anajua kuwa tunafanya video ili location alipoona sasa zile picha nini akaona ‘ohoo nisije nikaibiwa’. Lakini baadaye akaelewa kwahiyo mambo yakaenda fresh.”

Msikilize zaidi Ommy hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents