Bongo Movie

Ukweli kuhusu picha za Aunt Ezekiel zinazomuonesha kwenye vazi la Bibi Harusi

Kuanzia jana zimesambaa picha za muigizaji mahiri wa filamu nchini Tanzania, Aunt Ezekiel zinazomuonesha akiwa amevaa nguo za Bibi Harusi katika ndoa ya kiislam na huku akiweka saini kwenye kitabu.

Picha hizo zimesababisha blogs na website nyingi kuandika kwa mashaka kuwa ni kweli msanii huyo ameolewa?

Hata hivyo kwa mujibu wa watu wa karibu na Aunt, msanii huyo bado hajaolewa rasmi lakini yupo kwenye hatua za mwisho zikiwemo kukusanya michango kwaajili ya kufanya send-off yake.

Wamesema sherehe hiyo inategemewa kufanyika hivi karibuni ambapo wamedai imepangwa kufanyika kwenye ukumbi uliopo kwenye hoteli ya Serena.

Katika mahojiano na kipindi cha Take One cha Clouds TV miezi ya hivi karibuni, Aunt aliweka wazi kuwa anatarajia kufunga ndoa mwezi November mwaka huu.

Alidai kuwa tayari ameshavalishwa pete ya uchumba na mpenzi wake aitwaye Sunday.

Kutokana na hatua hiyo sasa muigizaji huyo amebadilisha dini na kuwa muislam na atakuwa akijulikana kama Rahma.

Ndoa yake inatarajiwa kufanyika uarabuni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents