Habari

Ukweli kuhusu miswaki (Chewing sticks) inayotokana na mimea

Utumiaji wa miswaki ya inayotokana na miti shamba (chewing sticks) kwa ajili ya kusafishia kinywa ina historia ndefu kutokana na tamaduni mbali mbali.

Ingawaje mimea yoyote ambayo sio sumu inaweza kutumika lakina watu wengi hupenda kutumia mimea aina ya Azadirachta indica na Vachelia nilotica ambayo imeonyesha uwezo mkubwa wa kuuwa bakteria na vimelea wengine waliopo mdomoni. Si mimea hii pekee tu inayotumika kama mswaki ipo mingi sana nchini.

Lakini katika tafiti nyingi zilizofanyika zinaonyesha mmea aina ya Salvadora Persia ndo unaopendwa sana na watu wwa maeneo mengi kwani unauwezo mkubwa wa kuzuia magonjwa ya kinywa na meno (dental carries, harufu mbaya na kung’oka kwa meno kwa wazee. Mmea huu umeonyesha uwezo mkubwa wa kuua bakteria.

Miswaki hii katika jiji la Dar es Salaam hupatikana kwenye masoko kwa bei ya shilingi 300 mpaka 500. Kwahiyo kwanzia leo kama hauna hela ya kununua dawa ya mswaki au upo maeneo ambayo upatikanaji wa bidhaa hii ni wa shida ni bora ni vyema ukatafuta mswaki unaotokana na miti shamba kwani ni upatikanaji wake ni rahisi na hauna madhara yeyote kiafya.

Your Health, Our Concern

NA FORD A. CHISANZA
Scientist/Researcher/Pharmacist
DAWAcall Tanzania
P.o.Box: 65529, Dar Es Salaam, Tanzania.
Mobile:+255 652466430/+255 684363584
Email: [email protected]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents