Habari

UKIMWI Virus Free Generation

Fid QKampeni kubwa inayotarajiwa kufanyika katika nchi mbali za Afrika na Ulaya kwa ujumla ikiwa inahusisha suala la Kizazi Kipya bila virusi inatarajiwa kufanyika na nchini Tanzania huku ikiwa imewahusisha wasanii wa nchi tano za Afrika na nne za ulaya, ambapo zitarekodiwa nyimbo kwa ushirikiano maalum wa nchi na nchi na msanii na msanii.

Fid Q

 

Kampeni kubwa inayotarajiwa kufanyika katika nchi mbali za Afrika na Ulaya kwa ujumla ikiwa inahusisha suala la Kizazi Kipya bila virusi inatarajiwa kufanyika na nchini Tanzania huku ikiwa imewahusisha wasanii wa nchi tano za Afrika na nne za ulaya, ambapo zitarekodiwa nyimbo kwa ushirikiano maalum wa nchi na nchi na msanii na msanii.

 

 

 

Akizungumza na Bongo5.com mteule pekee aliyechaguliwa nchini msanii Farid Kubanda a.k.a Fid Q alisema kuwa yeye anatarajia kupiga mkono mmoja na msanii Prinz P kutoka nchini Ujerumani, na hii itakuwa ni baada ya Maprodyuza kutengeneza mabiti tofauti ambayo yatachezwa na kituo cha redio cha Clouds FM kasha Mimi na Prinz tutachagua tukamulie ipiĀ” .

 

 

 

Utaratibu ambao unatarajiwa kutumika ni Maprodyuza watatengeneza mikono ambayo si Fid wala Mjerumani Prinz atakayekuwa akiifahamu then kitateuliwa kipindi maalum kwa ajili ya wakali hao kuchagua biti ya kukamulia, na yote hii ikiwa ni mapambano dhidi ya gonjwa hatari la UKIMWI Virus Free Generation (Vijana Bila Virusi).

 

 

 

Maprodyuza wataanza kupeleka mabiti kuanzia tarehe 28 mwezi huu na shughuli za kampeni hiyo zinatarajiwa kuanza tarehe 3 mwezi ujao na mpaka kufikia tarehe 5 itakuwa imekamilika kuanzia kufanya work shop, kurekodi nyimbo pamoja na kufanya tamasha.

 

 

 

Nchi zilizoshiriki na wasanii katika mradi huo Kwa Afrika ni pamoja na Tanzania, Zimbabwe, South Africa, Malawi, Namibia, na kwa ulaya ni Italy, Czech Republic, Holland na Germany. Ni kitendo cha kujivunia kwani inaweza kuonekana kuwa hata Tanzania kuwa wasanii wenye kila sababu ya kushiriki katika kampeni kama hizi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents