Habari

Ujio wa Obama nchini Kenya waacha historia, watoto waliozaliwa siku aliyowasili waitwa Barack Obama na wengine ‘AirForceOne’

Ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama umeacha historia ya mambo mengi kwa wananchi wa Kenya.

airforce one

Baadhi ya wazazi wa watoto waliozaliwa siku ambayo Obama alitua nchini Kenya Ijumaa ya July 24, wamewapa watoto wao majina yanayohusiana na Rais huyo.

Mzazi mmoja aliyejifungua mtoto wa kiume siku hiyo aliamua kumpa mtoto wake jina la Rais huyo. Sio jina la Rais peke yake ambalo mtoto huyo alipewa, bali na jina la ndege anayotumia, yaani jina kamili la mtoto huyo ni ‘AirForceOne Barack Obama’

mama airforce 1

Mama wa AirForceOne Barack Obama, Lucy Akinyi Okoth aliiambia AFP kuwa ameamua kumpa jina hilo mwanaye ili kukumbuka ujio wa Obama nchini Kenya kwasababu anaamini ni Baraka kubwa.

Mzazi mwingi alimuita mwanaye AirForceOne. Mama wa mtoto huyo Lucy Atieno, alisema kuwa ameambiwa kuwa hiyo ni ndege kubwa na bora kwasababu inambeba kiongozi mkubwa wa Marekani ambaye ni Mkenya.

mama michelle

Mtoto mwingine alipewa jina la mtoto wa Obama, Malia, huku mwingine akipewa majina ya watato wote wawili wa Obama, Malia Sasha. Yupo mwingine aliyeitwa jina la mke wa Obama, Michelle.

Hao ni wachache kati ya watoto wengi ambao walipewa majina yanayohusiana na Barack Obama.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents