Habari

Ujerumani: Sarafu kubwa ya dhahabu yenye dhamani $4m yaibiwa (Video)

Sarafu kubwa iliyotengenezwa kwa dhahabu, ambayo ina picha ya Malkia Elizabeth wa Uingereza, ambayo inakadiriwa kuwa na thamani ya $4m (£3.2m), imeibiwa kutoka kwenye makumbusho Ujerumani.

https://youtu.be/W48H8NVURBg

Sarafu hiyo kutoka Canada imeandikwa kuwa ya thamani ya $1m, lakini kwa sababu imetengenezwa kwa kilo 100 za dhahabu, thamani yake ni ya juu sana kwa kutumia bei ya sasa ya dhahabu.

Haijabainika ni vipi wezi walifanikiwa kuingia bila kugunduliwa na mtambo wa kuzuia wezi, na kisha wakafanikiwa kutoroka na sarafu hiyo ambayo nusu kipenyo chake ni cha nusu mita.

Wizi huo unaaminika kutekelezwa mwendo wa saa tisa unusu alfajiri Jumatatu.

Sarafu hiyo inadaiwa kuwa nzito sana kiasi kwamba mtu mmoja hawezi kuibeba.

Polisi wa eneo hilo wanasema huenda polisi waliingia kupitia dirisha.

Ngazi ilipatikana imetupwa kwenye reli iliyo karibu, msemaji wa polisi Winfrid Wenzel aliambia Reuters.

“Sarafu hiyo ilikuwa imehifadhiwa ndani ya sehemu isiyoweza kupenya risasi ndani ya makumbusho,” alisema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents