Michezo

Uingereza yaendelea kutia aibu kwenye Uefa, Man City wakubali kichapo kwa AS Monaco

Timu za Uingereza zimeendelea kutia aibu katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya (Uefa). Usiku wa jana (Jumatano) Manchester City wametolewa katika michuano hiyo na AS Monaco ya Ufaransa.

Katika mchezo huo Monaco waliokuwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Stade Louis II walifanikiwa kushinda kwa magoli 3-1. Magoli ya Monaco yalifungwa na Mbappe dakika ya nane, Fabinho dakika ya 29 na Bakayoko dakika ya 77 huku goli la kufutia machozi la City lilifungwa na Sane dakika ya 71.

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa wiki mbili zilizopita Man City wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani walishinda kwa mabao 5-3 na kufanya matokeo ya jumla kuwa 6-6. Nayo Atletico Madrid wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani walitoka sare ya bila kufungana na Bayern Leverkusen. Hata hivyo Atletico wamefuzu katika hatua ya robo fainali baada ya mechi ya kwanza kuibuka na ushindi wa mabao 4-2.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents