Bongo Movie

Uigizaji wamzuia Aunt Ezekiel kukaa na mumewe Dubai

Muigizaji wa filamu nchini, Aunt Ezekiel amesema kilichomfanya ashindwe kukaa Dubai na mume wake ni kazi ya uigizaji ambayo anaitegemea na hataki ipotee maishani mwake.

ez-2-333x333

Akiongea na Bongo5 leo, Aunt amesema kutokana na kazi yake kubwa anayoitegemea katika maisha yake ya kuigiza filamu, na soko lake lipo Tanzania itamwia vigumu kukaa Dubai kwa mumewe.

Hata hivyo ameongeza kuwa atakuwa anafanya kazi zake za filamu hapa nchini na kurudi Dubai kwa mume wake.

“Sasa nikisema nikae Dubai muda wote ni lazima kipaji changu kitapotea, hivyo nafanya kazi zangu kwa kutengeneza filamu kama tatu, kisha narudi Dubai kidogo kukaa na mume wangu,” Alisema Aunt.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents