Habari

Uhusiano wa Tanzania na Msumbuji uko vizuri – Serikali

Licha ya habari ya Watanzania kufukuzwa nchini Msumbiji kwa kukosa vibali, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Suzan Kolimba amesema nchi za Tanzania na Msumbiji zina uhusiano mzuri.

Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza katika kipindi cha JAMBO kinachorushwa na TBC mapema leo.

“Niseme tu mahusiano kati ya Tanzania na Msumbiji bila kujali ni mtu wa serikali tu anasema hata wanachi wa kawaida wale waliopo jirani na Msumbiji kwa maana Mtwara na hata kwa upande wa Msumbiji wanajua mahusiano yetu sisi yako vizuri,” amesema. “Ni mahusiano ya kindugu, ni mahusiano ya kirafiki lakini jambo hili lilivyotokea na linavyoelezewa na wale raia ambao wamekamatwa na kurudishwa Tanzania tumeona kwamba ni jambo la ajabu na ndio maana sisi kama wizara tuliamua kwamba tumuite balozi na kumueleza masikitiko ya Tanzania kwa jinsi jambo hili lilivyo tendeka, lakini mahusiano yetu kabisa yako vizuri kabisa,” amesisitiza.

Aidha Dkt Kolimba alisema walipokea taarifa kutoka kwa balozi wa Tanzania nchini Msumbiji kuwa pamoja na hayo yote walitoa muda wa siku 15 kwa watu wasio na vibali waondoke kwa utaratibu huo.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents