Burudani

Uhuru wa Afrika Kusini wamuomba Diamond afanye nao Remix ya wimbo wake mpya

Wimbo na video mpya ya Diamond ft. Mr. Flavour wa Nigeria imekuwa na mapokezi makubwa hata kwa mastaa wakubwa wa Afrika, ambao wamempongeza kwa wingi kupitia mitandao ya kijamii.

diamond2

Miongoni mwa mastaa hao ni pamoja na member wa kundi la Uhuru la Afrika Kusini ambaye pia ni producer, Dj Maphorisa ambaye amemuomba Diamond afanya nao Remix ya ngoma hiyo.

Dj Maphorisa ambaye ameshatengeneza hits nyingi za wasanii wengi wa Afrika wakiwemo Mafikizolo, Davido, Wizkid na Watanzania kama Linah, Madee, Chege na Temba, amepost comment aliyojibiwa na Diamond baada ya kucomment kwenye post yake ya Instagram na kuandika kuwa Diamond amekubali kufanya naye remix ya wimbo huo.

maphorisa2

Hii ndio ilikuwa comment ya Dj Maphorisa kwa Diamond
maphorisa diamond

Na hiki ndicho Platnumz alijibu:
diamond na uhuru insta

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents