Uhuru Mabingwa

Uhuru Mabingwa
Fainali za kombe la NSSF zilizofanyika kwenye viwanja vya TCC Sigara
Chang’ombe jana ziligeuka uwanja wa mapambano kati ya wabunge wa CCM,
katika fainali hizo ambapo zilikuwa zikicheza timu mbili za vyombo vya
habari ambazo ni Uhuru Publication na New Habari Corporation.


Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa vuta nikuvute kulitokea mashindano makubwa ya wabunge ambao ni Mh Rostam Azizi, Dr. Harrison Mwakyembe, mwanamama Anne Kilango na Katibu Mkuu wa Chama hicho mzee Yusufu Makamba.

Mpambano huo kati ya wabunge hao ulianza baada ya Mbunge na mmiliki wa kampuni ya New Habari Corporation Rostam Azizi kutuma ujumbe kwa mmoja wafanyakazi wa kampuni hiyo Muhingo Rweyemamu na kuahidi kuipa timu yake shilingi milioni 2 mbali ya zawadi itakayotolewa na NSSF endapo itaifunga Uhuru Publication, tangazo hilo lilipotangazwa ndipo naye Dr. Harrison Mwakyembe alipotuma ujumbe wa kuipa timu ya Uhuru Publication Shilingi milioni 6 kama wataishinda New Habari.

Mpambano wa Wabunge hao haukuishia hapo naye mama Anne Kilango aliahidi kuipa Uhuru Publication Milioni 2 na hatimaye katibu mkuu wa CCM Yusuf Makamba aliahidi kuipa timu hiyo shilingi Milioni 1 ikiwa itachukua ubingwa, ahadi hizo zilionekana kuwapa nguvu Uhuru ambao walicheza kwa kujituma na kujipatia magoli matatu kupitia kwa wachezaji wake Emanuel Mushi, Jamal Rashid na Tuzo Jackson.

Hivyo wakajizolea milioni mbili na nusu na kikombe pamoja na shilingi milioni 9 ambazo ziliahidiwa na wabunge Dr. Harrison Mwakyembe, Anne Kilango na Yusuf Makamba na kwafanya waibuke na kitita cha shilingi milioni 11.5.

Goli pekee la New Habari limefungwa na mchezaji Said Makala na kuondoka na shilingi milioni 2 na kikombe, katika fainali hizo pia kwa mchezo wa netiboli zilicheza timu za Business Printers na NSSF ambapo NSSF waliibuka mabingwa katika mchezo huo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents