Uchaguzi TFF Wajumbe Haoo Dar

WAJUMBE mbalimbali wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wanaanza kuwasili leo, alisema Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Fredrick Mwakalebela.

WAJUMBE mbalimbali wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wanaanza kuwasili leo, alisema Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Fredrick Mwakalebela.
“Mpaka sasa tayari maandalizi yote kwa ajili ya uchaguzi huo yamekamilika na wajumbe wataanza kuwasili leo.”
Akizungumza na waandishi wa habari jana Mwakalebela alisema wajumbe hao watafikia katika hotel ya Trevertine iliyopo magomeni na kesho kutafanyika mkutano mkuu ambao utazungumzia maswala mbalimbali ya uchaguzi mkuu.
Alisema tayari kamati mbalimbali zimeundwa na kamati ya uchaguzi kwa ajili ya kuendesha mkutano huo na Mkoa wa Dar es salaam umepewa hadhi ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo.
“Tayari maandalizi kwa kiasi kikubwa yamekamilika na wageni wataanza kufika kesho (leo) na sisi kama sehemu ya mkutano huo tunaamini mambo yote yatakwenda kama yalivyopangwa kwani lengo la uchaguzi huu ni kuleta maendeleo ya mpira wa miguu kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla,”Alisema Mwakalebela.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha soka Mkoa wa Dar es salaam DRFA, Amir Bharesa alisema wamejiandaa kwa ajili ya mkutano mkuu utakaofanyika kesho na siku ya uchaguzi huo.
Alisema wajumbe hao ambao wanatarajia kuwasili leo anaamini wamekuja kwa lengo la kubadilisha maendeleo ya mpira wa miguu na watachagua viongozi wanaoona wataweza kuuongoza shirikisho la mpira wa miguu na ambao wataleta mabadiliko makubwa katika soka la Tanzania.
Alisema jumla ya wajumbe 116 wanatarajia kushiriki katika mkutano huo na baadae katika uchaguzi utakaofanyika kesho kutwa Jijini Dar es salaam.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents