BurudaniDiamond Platnumz

Ubabaishaji AFRIMMA: Sheddy Clever alitangazwa kashinda, wakampa Oskido, Diamond alishinda 2, wakabadilisha ikawa 1

Waandaji wa tuzo za AFRIMMA wanaonekana walikuwa hawajajipanga vizuri kiasi cha majina ya washindi kubadilishwa wakati huo huo tuzo zikitolewa.

Diamond a_full

Diamond ameongea na waandishi wa habari baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo asubuhi na kuelezea ‘madudu’ hayo. Staa huyo amesema jukwaani alitajwa kuwa mshindi wa tuzo mbili ya Msanii Bora wa kiume Afrika Mashariki na Wimbo Bora wa kushirikiana (My Number One Remix Feat. Davido), lakini baadae yalifanyika mabadiliko na tuzo hiyo kupewa Mafikizolo na wimbo wa Khona waliowashirikisha Uhuru

“Hata producer ambaye alikuwa ametangazwa ameshinda ni Sheddy Clever kwa sababu walimuonesha mpaka anapiga kinanda, maclip yake. Kama waliweza kuedit hata vinanda vyake anapiga yuko studio ina maanisha yeye ndiye alikuwa ameshinda. Na wakatangaza collabo bora la kwangu mimi na Davido. Kwa sababu tuzo hii ndiyo tulienda kupewa kwenye stage kabisa pale. Lakini nyingine zilitangazwa kwenye TV,” alisema.

“Lakini ghafla, mpaka kesho yake tukauliza mbona hatupewi tuzo zetu mpaka sasa hivi. Kwa sababu hata dada Jide naamini anaweza kupata leo au muda mfupi leo. Sasa baadae wakaanza kusema kuna vitu vilikosewa sijui nini na nini…sikutaka tena kucomplain, kwa sababu nimeshapata yangu hii sikutaka kuleta matatizo mengine.”

Kwa maelezo hayo, Diamond alishinda tuzo moja peke yake.

Chanzo: Times FM website

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents