Habari

UAE yaunda wizara mpya za serikali ‘furaha’ na ‘uvumilivu’

Waziri mkuu wa Miliki za Kiarabu UAE ametangaza kuundwa kwa wizara mpya ya furaha, uvumilivu pamoja na vijana huku akiahidi kuunda wizara nyingi zaidi.
160209121507_sheikh_mohammed_bin_rashid_al_maktoum_prime_minister_and_vice-president_of_the_united_arab_emirates_and_ruler_of_dubai_640x360_afp_nocredit

Wizara hizo mpya imeundwa katika mabadiliko yaliyotekelezwa na utawala wa kiongozi wa UAE Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum.

Sheikh Maktoum, ambaye ni kiongozi wa Dubai amesema wizara mpya ya furaha inaazimiamia “kuchochea mtagusano baina ya wananchi wake mbali na kuhamasisha umma utosheke na kile walichonacho”.

Wizara mpya nyingine iliyoundwa ni “wizara ya kuvumiliana.”

Sheikh Maktoum vilevile ameagiza kuunganishwa kwa wizara nyingi mbali na kutoa zabuni za kuagiza makampuni kutoka nje kuendesha asilimia kubwa ya shughuli za serikali.

“Serikali sharti iweze kunyumbulika kwa urahisi. Nafikiiri hatuitaji wizara zaidi tunachoitaji ni mawaziri wenye uwezo wa kutafsiri mabadiliko na kuatekeleza ipasavyo” Sheikh Makhtoum aliiambia kongamano la dunia linalojadili miundo ya utawala na serikali mjini Dubai.

“Tunachotaka ni serikali changa itakayokidhi matakwa ya vijana na umma.”

Wizara ya uvumilivu inanuiwa kupalilia nguzo muhimu ya jamii ya raia wa miliki za kiarabu ” alisema Sheikh Makhtoum kupitia mtandao wake wa Tweeter.

Vijana pia hawakusaulika aliunda baraza la vijana la taifa ‘Youth National Council’.

Wajibu wao mkubwa ni kuishauri serikali kuhusiana na maswala yanayowahusu vijana na wataongozwa na waziri mwanamke ambaye umri wake hautazidi miaka 22.

“Vijana ndio utawala ujao wa taifa hili” aliongozea Sheikh Makhtoum

Source:BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents