Habari

Tyrese: Nahitaji kufanya movie nyingine na Taraji


Unaikumbuka filamu maarufu sana ya Baby Boy (2001) aliyoigiza mwanamuziki Tyrese, rapper Snoop Dogg na muigizaji maarufu Taraji P Henson?

Katika filamu hiyo Tyrese ameigiza kama Jody (20) anayeishi na mama yake Juanita. Tyrese ameigiza kama mtoto wa mama fulani ambaye haoneshi dalili ya kuwa mtu mzima na kukabiliana na majukumu kama baba baada ya kumzalisha mpenzi wake Yvette (Taraji P. Henson) mtoto wa kike aitwaye Peanut.

Kwa muda mrefu watu wamekuwa wakisubiri sana ujio mpya wa filamu nyingine itakayowakutanisha wawili hao. Leo (June 2) Tyrese kupitia Twitter ameonesha kuwa yeye pia ana hamu ya kukutana na Taraji. “I need to do another movie with this woman …. Fast … Where is my baby.?” Ametweet akiambatanisha picha waliyopiga pamoja.

Tweet hiyo inatupa maswali mengi hasa anapoandika’ Fast’ kwasababu tunajua kuwa awamu ya sita ya filamu maarufu ya Fast and the Furious ambayo Tyrese yumo kwenye zote tano zilizopita, huenda Taraji akaonekana humo pia! You never know!

Mwezi July mwaka jana Tyrese alitweet pia kwa kuandika, “Official.. Me and my girl Taraji are doing another classic together soon.!! John Singleton will be directing us. And it’s not BB2.”

Vyovyote itakavyokuwa, Taraji na Tyrese wanapendeza sana kuwa kwenye movie moja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents