Burudani
Tyrese Gibson akiri kuwa yuko ‘in love’ na Lupita Nyong’o
Mwimbaji wa R&B na muigizaji wa Fast and Furious, Tyrese Gibson ameamua kuonesha hisia alizonazo juu ya muigizaji wa 12 Years a Slave, Lupita Nyong’o, kwa kukiri kuwa anampenda na kumtamani.
Tyrese aliutumia mtandao wa Instagram kuonesha hisia zake kwa Lupita kwa kupost picha ya mrembo huyo iliyoambatana na maneno machache, “I’m in lust and love”.