Burudani

Tyga akanusha tetesi za kuwa na uhusiano na Kylie Jenner (mdogo wa Kim K) mwenye miaka 17

Baada ya rapper Tyga kuachana na baby mama wake Blac Chyna miezi miwili iliyopita, kuna tetesi kuwa rapper huyo ameanzisha uhusiano mpya wa kimapenzi na mdogo wake Kim Kardashian aitwaye Kylie Jenner mwenye miaka 17.

Kylie2

Lakini kama ilivyo kawaida ya mastaa wengi, Tyga (24) amekanusha kwa kusema tetesi hizo si za kweli, na kusisitiza kuwa hana uhusiano wowote na mtoto huyo mrembo Kylie, zaidi ya urafiki wa kawaida alionao na familia yao.

“DON’T BELIEVE THE RUMORS, BEEN FRIENDS WITH THE FAMILY FOREVER. WERE [sic] ALL JUST FRIENDS,”
Alitweet Tyga.

Blac Chyna alikuwa rafiki mkubwa wa Kim Kardashian kiasi cha kufanya familia zao ziwe na ukaribu.

Kylie
Kylie

Tetesi za Tyga na Kylie kuwa wapenzi zimeedelea kupata nguvu zaidi wiki hii baada ya wawili hao kuonekana wakipata dinner kwa mara ya pili katika mgahawa mmoja wa Kijapan huko Hollywood Jumatatu wiki hii. Hii ni baada ya kuonekana kwenye dinner ya kwanza wiki iliyopita huko Sherman Oaks.

Tyga & Kylie2
Tyga na Kylie wakitoka dinner

Wakati bado mambo hayajapoa Tyga alipost picha nyingine jana akiwa na Kylie na Big Sean.

Tyga-sparks-Kylie-Jenner-rumours
Tyga, Kylie na Big Sean

US Weekly pia iliripoti kuwa Tyga na Kylie wamekuwa wapenzi wa siri toka mwezi wa nane toka Tyga alipotengana na Blac Chyna.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents