Habari

Twanga Pepeta kuzindua wimbo uliotungwa na Kalala Junior


Baada ya kuondoka kwenye kundi la Mapacha Watatu na kurejea African Stars, Twanga Pepeta, muimbaji Kalala Junior ametunga wimbo mpya utakaozinduliwa hivi karibuni kama ishara ya kumkaribisha nyumbani.
Wimbo huo uitwao Nyumbani ni Nyumbani utazinduliwa sambamba na utambulisho wa muimbaji huyo aliyerudi kundini kwenye onesho maalum litakalofanyika ijumaa hii jijini Dar es Salaam.
Wiki iliyopita Kalala Junior aliwaambiwa waandishi wa habari kuwa Nyumbani ni Nyumbani ni wimbo ambao ameuandika kuzungumzia masuala mbalimbali aliyokutana nayo katika muziki mpaka kuchukua uamuzi wa kuitosa Mapacha Watatu na kurejea Twanga Pepeta.
Muimbaji huyo ambaye jina lake halisi ni Kalala Hamza Kalala, alisema ameamua kurejea Twanga Pepeta kwa mapenzi yake mwenyewe pasipo kulazimishwa na mtu kwakuwa bendi hiyo ndiyo iliyompa umaarufu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents