Michezo

Tuzo za KTMA 2014 zazinduliwa, zaja na mabadiliko

Tuzo za muziki Tanzania, Kilimanjaro Tanzania Music Awards zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam.

IMG_3091
Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akiongea kwenye uzinduzi huo

Akiongea kwenye uzinduzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano uliopo kwenye hoteli ya Kebbys, meneja wa bia ya Kilimanjaro George Kavishe amesema baada ya kufanya utafiti wa kina mwaka jana, wameamua kufanya maboresho zaidi katika mchakato wa kupata majina ya waimbaji watakaowania vipengele mbalimbali.

“Tuzo zinaendelea kukua kila mwaka kuendana na matakwa ya tasnia ya muziki wa Tanzania,” alisema Kavishe.

Kavishe amesema mabadiliko yaliyofanyika mwaka huu ni Watanzania kupewa nafasi ya kupendekeza wenyewe majina ya waimbaji watakaowania vipengele 34 vinavyoshindaniwa mwaka huu. Awali majina yote yaliyokuwa kwenye vipengele mbalimbali yalikuwa yakipendekezwa na academy.

Kavishe amesema mwaka huu academy itafanya kazi ya kuhakikisha tu majina ya waimbaji waliopendekezwa na wananchi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Mtendaji Baraza la Sanaa Tanzania, BASATA Geodfrey Ngereza alisema ana imani kuwa tuzo za mwaka huu zitakuwa bora zaidi kuliko za miaka iliyopita.

Akielezea mabadiliko mengine yaliyofanyika kwenye tuzo hizo, mratibu wa tuzo hizo kutoka BASATA, Maregesi Ng’oko Kulwijira amesema kipengele cha Mtayarishaji Chipukizi kimeondolewa. Ameongeza neno ‘Msaani’ kwenye majina ya vipengele limebadilishwa na kuwa ‘Mtumbuizaji’ na Mwimbaji’ kwakuwa Msanii lina maana nyingi.

Tuzo za mwaka huu zitakuwa na jumla ya vipengele 36 ambapo 34 zitakuwa za kupigiwa kura na 2 ni za watu ama kikundi kilicholeta mabadiliko au mchango mkubwa kwenye tasnia ya muziki nchini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents