Burudani

Tusker Project Fame 5 kwenda ‘digital’ na Samsung

Tusker Project Fame 5 imepata udhamini mnono kutoka Samsung Electronics East Africa ambao utayafanya mashindano hayo yaingie kwenye ulimwengu wa digital.

Kama sehemu ya makampuni hayo mawili kuadhimisha siku ya mazingira duniani mwaka huu, Samsung Electronics itatoa vifaa vya digital vitakavyotumiwa na washiriki, majaji na walimu kwenye mashindano hayo.

Ili kurahisisha mawasiliano zaidi washiriki, majaji na walimu katika TPF 5 watapewa Galaxy Tabs, na simu za Galaxy Pocket.

Vifaa hivyo vitatumika pia kama njia ya washiriki kupokea maelekezo na kujibu kwa haraka ili kupunguza matumizi ya karatasi.

Washiriki wote watapewa camera za digital za Samsung (picha na video) kurekodi maendeleo yao kwenye nyumba ya TPF.

Katika mashindano ya mwaka huu ya TPF 5, timu ya walimu inayoongozwa na Hellen Mtawali itatoa kwa urahisi kazi za darasani na maelekezo mengine kwa kutumia Galaxy Tablets.

Majaji wakiongozwa na Ian Mbugua watatoa pia hukumu zao kwa kutumia vifaa hivyo vya kisasa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents