Burudani

Tundaman: Mimi ndio nilikuwa na kosa, kwa sasa sina tofauti na Tale

Tundaman amefunguka kuwa kwa sasa yeye na Babu Tale hawana matatizo tena kama zamani.

Mwezi Disemba mwaka jana, hitmaker huyo wa ‘Mama Kijacho’ aliiambia EATV kuwa amekuwa hapati support kutoka kwa Tale ambaye ni meneja wa kundi la Tip Top Connection huku kazi kubwa ya kusimamia kazi zake akiifanya mwenyewe.

Akiongea na mtangazaji wa Maisha FM ya Dodoma, Silver Touchez, Tunda amesema, “Nakiri mimi nilikosea, kosa lilikuwa kwangu kwa hiyo kila kitu kimeshaisha haina haja tena kuzungumza tena. Kwa sasa hatuna tofauti tena japo mwanzo zilikuwepo.”

Tunda ameongeza kuwa kwa mwaka jana usimamizi wa Babu Tale katika kundi hilo ulikuwa mdogo lakini kwa mwaka huu wameahidiwa kila kitu kitakuwa sawa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents