Habari

Tundaman kuachia video mpya iliyomgharimu mamilioni

Pata picha kwenye video ya muziki wanaonekana Jackline Wolper, Lulu (muigizaji aliyepo mahabusu kwa tuhuma za kusababisha kifo cha Steven Kanumba), Shilole, Anti Ezekiel, Diamond, Mo Racka na wengine!

Awamu hii Tundaman hataki mchezo na amefumba macho kwa gharama yoyote ile ili kupiga kioo (video) cha ukweli na nyota hao wote hapo juu wataonekana.

Kwa mujibu wa Tundaman hiyo ni video ngumu, iliyochukua muda mrefu na yenye gharama kubwa kuliko zote alizowahi kufanya.

Baada ya kusuburia kwa hamu video hiyo iliyofanywa na Adam Juma, director mwenye kazi nyingi za aina hiyo pengine kuliko wote nchini, ijumaa hii itatambulishwa rasmi.

Video imetumia muda mrefu kutokana na mchakato mzima wa kutafuta watu watakaoonekana ndani ambao wengi wao ni watu maarufu na walio busy na mambo mengi.

Video hiyo ni ya wimbo wake uitwao ‘Dem Sio’ unaomzungumzia msichana mwenye tabia (mbaya) tofauti na wasichana wengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents