Burudani

Tunda Man, Mr Blue, Snura na Ali Choki kupamba tamasha la bure la ‘Amsha Mama’

Wasanii wa muziki Mr Blue, Snura na Ali Choki pamoja na balozi wa tamasha la ‘Amsha Mama Tanzania’ Tunda Man wanatajia kufanya show ya bure katika tamasha la ‘Amsha Mama’ litalofanyika Machi 5 mwaka huu katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es salaam.
Tunda Man

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Ijumaa hii, Mkurugenzi wa Kampuni ya Candy & Candy record yenye makao makuu yake nchini Kenya ambao ndio waandaaji watamasha hilo, Joe Kariuki alisema ameamua kulileta tamasha hilo nchini ili kuwapa fursa ya akina Mama ya kupata elimu.
.

“Akina mama mjitokeze kwa wingi katika tamasha hili mahususi kwenu kwa kuwa mtapata fursa mbalimbali za kujifunza na mtaweza kupata mambo mbalimbali ya kuweza kuwaongoza katika biashara zenu,” alisema Kariuki.

Kwa upande wake balozi wa ‘Amsha Mama’ nchini Khalid Ramadhani ‘Tundaman’, amewaomba akina mama kuchangamkie fursa hiyo kwani watajifunza mambo mengi.

“Nawaomba Mama zangu mjitokeze kwa wingi kwani tumepata bahati ya pekee ya kuletewa tamasha nchini,” alisema Tunda.

Aidha, Kairuki alisema tamasha kubwa linatarajiwa kufanyika katika jiji la Naivasha nchini Kenya Machi 25 hadi 27 huku likitarajia kuwa kutanisha akina Mama kutoka nchini zote za Afrika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents