Tunawasaka waliovamiashamba la Balali – Polisi

Polisi mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, wanamsaka mtuhumiwa na washirika wake walioandaa mpango wa kuvamia shamba la gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dk. Daudi Balali lililoko Mbweni-Maputo, nje kidogo ya Dar es Salaam.

Na Khalfan Said



Polisi mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, wanamsaka mtuhumiwa na washirika wake walioandaa mpango wa kuvamia shamba la gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dk. Daudi Balali lililoko Mbweni-Maputo, nje kidogo ya Dar es Salaam.


Akizungumza na gazeti hili jana, Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Bw. Jamal Rwambow, alisema polisi imeanzisha msako wa kumtafuta aliyepanga mpango huo na washirika wake ili wafikishwe mahakamani kwa kosa la kuvamia eneo lisilo lao.


Kamanda alisema imethibitika kuwa ardhi waliyovamia iliyoko kijiji cha Maputo ni mali ya Dk. Balali.


“Hadi sasa hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio la uvamizi wa ardhi ya gavana wa zamani wa BoT,“ alisema.


Wavamizi hao walijitosa ndani ya shamba la Dk. Balali mwishoni mwa wiki na kujigawia wakidai kuwa alipata mali hizo kidhalimu wakihusisha madai ya ubadhirifu wa Sh. bilioni 133 ndani ya Benki Kuu zilizolipwa kwa makampuni yasiyokuwa na stahili.


Kamanda Rwambow alisema taarifa za kuvamiwa zilifikishwa kwake na diwani mmoja aliyemtaja kwa jina la Mbonde
“Niliarifiwa na diwani Mbonde kuwa kundi la watu wanafanya uvamizi kwenye ardhi ya Balali na nilipotuma vijana wangu wale watu walitawanyika,“ alisema Kamanda Rwambow.


Alisisitiza kuwa polisi haina mpango wa kuweka ulinzi kwenye eneo hilo na jambo linaloweza kufanyika ni kuwasaka wahusika.


Kamanda Rwambow hakutaja ukubwa wa ardhi yenyewe ingawa alisema ameelezwa kuwa ni eneo kubwa.


Mkazi wa Maputo Bw. Mfaume Khamis, alisema juzi kuwa sehemu hiyo ni pori lenye ukubwa wa karibu hekta 15 na kwamba kilichojengwa hapo ni kibanda cha mlinzi na wanachokiona porini hapo nyoka na wadudu wengine.


Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents