Tunamsaka Miss Kigamboni 2009

Tunamsaka Miss Kigamboni 2009
Wadau wa Bongo5, tunapenda kuwatangazia ya kwamba mwaka huu kampuni yetu ya Bongo5 Media Group imeamua kuandaa taji la kumtafuta Miss Kigamboni inayotarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi wa nne.

Mratibu wa mashindano hayo ambaye ndio mkurugenzi wa Bongo5, Luca anasema ya kwamba mashindano ya mwaka huu ya kumtafuta mrembo wa Kigamboni yatakuwa ya aina yake kwakuwa wamejipanga vyema na wanaamini kwamba lazima Miss Tanzania atokee Kigamboni.

Form za kushiriki kwenye mashindano hayo zinapatika kwenye ofisi za Bongo5 zilizopo karibu na Posta Mpya mtaa wa Jamhuri na pia zinapatikana online kwa kubofya hapa.

SIFA ZA MSHIRIKI:

1.       Awe na umri si chini ya miaka 18 na umri usiozidi miaka 24.

2.       Awe raia wa Tanzania.

3.       Awe hajaolewa .

4.       Awe na ufahamu wa kutosha wa kujieleza.

5.       Awe hajazaa.

6.       Asiwe mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari.

7.       Asiwe amekwisha shiriki mashindano ya Miss Tanzania katika ngazi yoyote mwaka huu 2009 (Yaani hairuhusiwi kushiriki mara mbili katika mwaka mmoja).

Mwisho wa kujaza na kurudisha fomu ni tarehe 8 April hivyo warembo wanaombwa kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye shindano hilo.

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na

+255715009099
+255786712222
+255713946403

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents