Habari

Tunahitaji zaidi ya kilichopo sasa kwenye game ya Hip Hop

Hip hop ni steji huru, ni aina muziki ambao asili yake ilijengwa katika misingi ya watu wa jamii hiyo kusema na kuelezea hisia zao juu ya wasanii wengine au mambo mbalimbali yaliyotokea. Muda mwingine kwa lugha kali na yenye kuudhi na pengine hiki ndicho kinafanya muziki wa Hip Hop uwe wa aina yake.

Msanii wa hip hop, Young Killer Msodoki ameachia ngoma yake, Sinaga Swagga, ni ngoma iliyoacha gumzo na kuzua mjadala kwenye media na mitandao ya kijamii. Hii ni kutokana na Young Killer kuwachana live wasanii kama Young Dee, Dogo Janja, Joh Makini. Labda kilichoshangaza ni kutokana na kuwa hakujakuwa na ngoma za aina hiyo kwa muda sasa kwenye hip hop ya hapa nyumbani.

Pamoja ya kuwa Young Killer ameonekana kama kugwaya kwa kujitetea kwa yale aliyoyasema kwenye Sina Swagga hasa kuhusu ishu ya Joh kubebwa na media, binafsi nimependa alichofanya Young Killer. Haijalishi kama naunga mkono yale aliyoyaongelea humo ama lah! Nilichopenda ni kuweza kuweka wazi yale ambayo wengine hawawezi kwa kuogopa ama kutengeneza bifu na wasanii fulani au kupoteza kundi la mashabiki linalomsapoti msanii huyo.

Binafsi yangu naamini hip hop inahitaji ngoma kama hizo,tunahitaji kuona battles, diss, majigambo, kitu ambacho upande wangu naona inachangamsha game na kuibua mijadala ambayo inaleta msisimko mkubwa kwenye game.

Nikimnukuu Godzilla aliwahi kusema urafiki wa wasanii wa hip hop umepunguza msisimko kwenye game. Ni kweli sasa ni ngumu kusikia wasanii wakichanana kama ilivyokuWa miaka ya nyuma kidogo. Diss lines ni moja kati ya vitu vinavyosisimua na kuleta mvuto wa kipekee, na vinavyotofautisha muziki wa hip hop na aina nyingine ya muziki, ni afya kwa hip hop as long as haileti matokeo hasi kama bifu na chuki binafsi.

Imeandikwa na Eliezer Gibson greencitynative

Instagram:gibson_elly

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents