Uncategorized

Tujitokeze kuchangia Diva for Charity


Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho, Loveness Luv, a.k.a Diva ameandaa kampeni ya wiki moja ya uchangiaji wa msaada kwa ajili ya kituo cha watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.
Kampeni hiyo ya uchangiaji ameipa jina la Giving for Charity ambayo inatarajiwa kufanyika siku ya Tarehe 9/12/2012 Pale Tandale katika Kituo Cha Almadina Children Home.
Kwa mujibu wa taarifa yake loveness luv, ametanabaisha Kituo cha Almadina kinaongozwa na Kuendeshwa na Bi.Kuruthum Yusuph Juma, ambaye ana Miaka 53 na ni mtu wa Mafia ila hapo kilipo kituo hicho amepanga na analipia shilingi za kitanzania mil 3 kwa Mwaka.
Diva anasema sehemu kilipo kituo hicho ni ndogo sana na mazingira ni magumu sana. Kuna jumla ya watoto 52 ambao ni yatima , ikiwemo wanaume 24 na Wanawake 28, na watoto watano waliomaliza Darasa la 7, ambao wanatakiwa kwenda sekondari.
Watoto waliopo shule ya msingi ni 33 , sekondari 8, na waliobaki wote ni wadogo hawajaanza chekechea.
Diva aliyataja mahitaji ya kituo hicho ni pamoja na mahitaji yote muhimu anayohitaji mtoto, hivyo ni muhimu Kuchangia na kupitia tigo Pesa 0655 879287.
Alimalizia kwa kusema, katika kufanikisha uchangiaji huo atashirikiana na THT Ambao nao wanatimiza miaka 7 siku kadhaa kutoka sasa na watatoa asilimia 20 ya mapato yao ili kusaidia kampeni ya Diva Giving for Charity kwa ajili ya watoto hao.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents