BurudaniDiamond Platnumz

Tudd Thomas asema alilipwa milioni 4 kutengeneza ‘Mdogo mdogo’ na ‘Ndagushima’, na ilimchukua zaidi ya miezi 3 kuzikamilisha

Inawezekana umeshawahi kusikia malalamiko ya maprodyuza wa muziki Tanzania kuhusu kutonufaika wanavyostahili kwa kazi wanazowatengenezea wasanii, kama zinavyowanufaisha wenyewe kupitia shows wanazofanya kwa kutumia nyimbo hizo.

tudd3

Lakini inaonekana kuna kafaida zaidi producer anapofanya kazi na wasanii wakubwa, ukiachilia mbali wimbo kupigwa sana na kumpa ‘credit’ mtengenezaji, lakini kuna uwezekano wa kuweka makubaliano ya malipo tofauti kulingana na ukubwa wa wimbo na hata ukubwa wa jina la msanii pia.

tudd2

Mfano mzuri ni kupitia kazi mpya ya Diamond ‘Mdogo mdogo’ na ya Ommy Dimpoz ‘Ndagushima’, ambazo zote zimetayarishwa na Tudd Thomas wa Surround Sound Studio. Tudd amesema alilipwa jumla shilingi milioni 4 kwa nyimbo zote mbili.

“Kikawaida huwa wanasema sio vizuri kwa kuwa ni biashara lakini mimi niko real, ni two million kwa kila wimbo.” Aliiambia Sunrise ya Times FM.

Pia ameongeza kuwa ilimchukua muda mrefu kuziandaa nyimbo hizo, ‘Mdogo mdogo’ ilimchukua miezi mitatu kutokana na idea hiyo kuwa mpya kwa Platnumz na kwake pia, na ‘Ndagushima’ alitumia miezi miwili.

Source: Times FM

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents