Burudani

Tudd Thomas afuata nyayo za Dr. Dre, kuingiza sokoni headphone zake ‘TTP’

Producer wa single mpya za Diamond ‘Mdogo mdogo’ na ‘Ndagushima’ ya Ommy Dimpoz, Tudd Thomas ameweka wazi kuhusu mradi wake mpya wa headphones zitakazokuwa na brand ya Beats By Thomas TTP, yaani ‘Tudd Thomas Production’.

tudd3

Akizungumza na tovuti ya TIMES FM, Thomas ameelezea jinsi wazo la mradi huo ambao uko jikoni lilivyozaliwa:

“Wakati mimi naanza kufanya production rasmi, alikuwepo mtu ambaye anatusimamia mimi na Marlaw anaitwa Ben Konzo, ana kampuni ya kutengeneza subwoofer na TV na simu zake. Kwa hiyo nilimfuata yule nikamuomba aweze kunielekeza.”

Ameendelea kusema:
“Kwa hiyo akanielekeza nini cha kufanya, ukiwa na mtaji hivi na hivi unaweza kufika hapa. Kwa hiyo nikatafuta income na mpaka sasa hivi nimeshazicreate zile headphones na wameshatutumia sample kwamba ‘je mnataka iwe hivi?’. Nikasikiliza sound haikwenda sawa na unavyotaka. Kwa sababu nataka headphone nayoitengeneza iwe na sound ambayo mimi naitaka, akisikiliza bongo fleva awe anaenjoy.”

Tudd ameongeza kuwa lengo lake sio tu kuingiza sokoni headphones, lakini headphones zenye ubora utakaokidhi aina ya sound ya muziki wa Bongo, ambayo yeye kama producer anajua kinachohitajika ili headphones hizo zikidhi viwango anavyotaka.

“Asilimia kubwa ya wanaotengeneza headphone ni watu kutoka nje, kwa hiyo huwa wanaifikiria sound yao wenyewe. Kwa hiyo nachokifikiria mimi naifikiria sound yetu sisi Africans, fusion…kwa sababu fanya vyovyote unavyofanya, muziki wetu sisi unasound tofauti na muziki wa Ulaya. Kwa hiyo naweka kile kitu ambacho kitakuwa best kwetu, tuenjoy sisi wenyewe.”

Source: Tovuti ya TIMES FM

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents